Wenye ujuzi please tufundishane kuchanganya icing sugar kwa ajili ya kupambia keki.

Kupika keki tamu kabisa nafahamu(shukran kubwa kwa shosti angu wa faida kwa kunipa utaalamu wa kupika keki) tatizo lipo kwenye kutengeneza mchanganyiko wa icing sugar. Nilishapewa somo la awali la kutumia ute wa yai ila nimeshindwa fata njia sahihi.

[ATTACH=full]178406[/ATTACH]

Ni laini sana na ni rahisi kuweka mabonge, unashauriwa uichekeche kwanza kwenye bakuli kabla hujaana kuchanganya na viungo vingine. Changanya na starch ya mahindi.
Uwiano kikombe 1 sukari = kikombe 1 starch.
Mchanganyiko huo unaupika ndani ya ute mweupe wa yai.

Ngoja nisubir ujuzi wa breakfast hapa

Zipo za aina mbili
ya kutumia mayai (royal icing)
ya kutumia butter.
napenda hiyo ya butter

mahitaji
.icing powder
.butter (blueband au mafuta ya kimbo)
bora mafuta make ni meupe ukitumia blue band icing yako inakua na rangi ya blueband
.Maziwa kidogo
.Flavour (vanilla)

Chekecha au pekecha kwa mikono icing hadi iishe vibonge bonge
wekea butter kisha changanya (kwa mwiko au mixer)
kama ni nzito ongezea maziwa pima kwa kijiko cha chakula
weka flavour yako few drops

vipimo
icing 300gm
butter 100gm
milk 3-4 table spoon
flavour few drops

Nb vipimo vinategemea uhitaji wako

Uko sahihi