Wanaume wa mara hatutekwi kizembe. (Picha)

chemical Ali

Senior Villager
#1
Safi sana zakaria inawezekana usiwe mkuria mgita and the likes lakini ushujaa wako uliouonyesha umetuwakilisha vyema wanaume wa kanda ya ziwa.. mara vita ni vita unnamed.jpg
 
June14

Senior Villager
#9
Kwa haya yanayoendelea basi hata yule tajiri mwingine wa mabasi aliyeokotwa ziwani sijui mtoni wahusika ni hawahawa jamaa.
 
King Kong III

Senior Villager
#12
Kwa haya yanayoendelea basi hata yule tajiri mwingine wa mabasi aliyeokotwa ziwani sijui mtoni wahusika ni hawahawa jamaa.
Baada ya jana Mwenyekiti wa UVCCM Tarime, Bw.Godfrey Francis kutoa taarifa kwamba watu waliomvamia Zacharia walikua na lengo la kumteka lakini akawazidi nguvu, halafu baadae RC Malima akaja na maelezo kwamba watu hao ni maafisa wa usalama wa taifa nimebaki nimeduwaa. Ukiunganisha taarifa hizi mbili (ya Mwenyekiti wa UVCCM na ya Mkuu wa mkoa) unapata ukakasi kuhusu idara ya usalama wa taifa. Nimejiuliza hivi Zacharia angetekwa kama inavyodaiwa, na watekaji wakafanikiwa kupotea nae bila kujulikana, je RC Malima angeweza kukiri kwamba watu hao ni maafisa wa idara ya usalama wa taifa?

Jaribio hili la kumteka Zacharia ambaye ni mmiliki wa mabasi ya Zacharia limenikumbusha tukio jingine la mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Ndugu Samson Josiah, ambaye alitekwa na watu wasiojulikana. Baada ya siku kadhaa gari yake ikaokotwa huko Serengeti ikiwa imechomwa moto, na baadae mwili wake ukaokotwa akiwa amechinjwa, kukatwa miguu yake na kuwekwa kwenye mfuko wa sandarusi kisha kutupwa Ziwani. Mmiliki huyu wa mabasi akauawa kikatili na hadi leo hakuna RC yeyote aliyejitokeza kusema watu hao ni kina nani? Laiti angewazidi nguvu.!!

Malisa GJ.

MJG.jpg MJG.jpg
 
Stroke

Senior Villager
#14
Ukipitia ile JF kuu; utakuta nyuzi kibao za lawama kuwa huyu mtu alikuwa anaachwa afanye atakavyo;

Baada ya hili kutokea wale wale ndio wamegeuka watetezi wake wakuu;

Wanasiasa wa upinzani na vibaraka wao ni wadandiaji wa matukio hawana lengo lolote jema kwa Taifa letu; ni wa kupuuzwa
 
tremendous

Village Elder
#16

Kwahiyo unafurahia watu kutekwa hata kama ni waovu kwanini asikamatwe na polisi kama kavunja sheria?
 
#17
Ukipitia ile JF kuu; utakuta nyuzi kibao za lawama kuwa huyu mtu alikuwa anaachwa afanye atakavyo;

Baada ya hili kutokea wale wale ndio wamegeuka watetezi wake wakuu;

Wanasiasa wa upinzani na vibaraka wao ni wadandiaji wa matukio hawana lengo lolote jema kwa Taifa letu; ni wa kupuuzwa
Hata kama Zacharia ana makosa si kuna taratibu za mtu kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria??
Wewe umeona ni sawa yeye kutaka kutekwa na hao watu wa usalama wa Taifa?
Unajiita Mwanasheria kumbe punguani tu.
 
June14

Senior Villager
#18
Baada ya jana Mwenyekiti wa UVCCM Tarime, Bw.Godfrey Francis kutoa taarifa kwamba watu waliomvamia Zacharia walikua na lengo la kumteka lakini akawazidi nguvu, halafu baadae RC Malima akaja na maelezo kwamba watu hao ni maafisa wa usalama wa taifa nimebaki nimeduwaa. Ukiunganisha taarifa hizi mbili (ya Mwenyekiti wa UVCCM na ya Mkuu wa mkoa) unapata ukakasi kuhusu idara ya usalama wa taifa. Nimejiuliza hivi Zacharia angetekwa kama inavyodaiwa, na watekaji wakafanikiwa kupotea nae bila kujulikana, je RC Malima angeweza kukiri kwamba watu hao ni maafisa wa idara ya usalama wa taifa?

Jaribio hili la kumteka Zacharia ambaye ni mmiliki wa mabasi ya Zacharia limenikumbusha tukio jingine la mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Ndugu Samson Josiah, ambaye alitekwa na watu wasiojulikana. Baada ya siku kadhaa gari yake ikaokotwa huko Serengeti ikiwa imechomwa moto, na baadae mwili wake ukaokotwa akiwa amechinjwa, kukatwa miguu yake na kuwekwa kwenye mfuko wa sandarusi kisha kutupwa Ziwani. Mmiliki huyu wa mabasi akauawa kikatili na hadi leo hakuna RC yeyote aliyejitokeza kusema watu hao ni kina nani? Laiti angewazidi nguvu.!!

Malisa GJ.

View attachment 180841 View attachment 180841
Walisema nchi tumewapa!!! Washamba kweli ni washamba, wapuuzi, wauaji.

Wanafanya haya halafu wanajikausha.
 
Top