Wamiliki wa blogu wawaaga wasomaji wao,TCRA yaongeza muda...

Saturday, June 16, 2018

[SIZE=7]Wamiliki wa blogu waaga wasomaji wao, TCRA yawaongezea muda[/SIZE]

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/4615172/highRes/2010858/-/maxw/600/-/eum1qu/-/pic+blog.jpg

[SIZE=5][FONT=times new roman]Kwa ufupi[/FONT][/SIZE]
[ul]
[li][FONT=times new roman]Wamewaaga watumiaji wa blogu hizo ambao walizoea kupata taarifa muhimu za Serikali na matukio mengine ya kijamii kwenye kurasa zao za mitandao ya intaneti.[/FONT][/li][/ul]
[FONT=times new roman]By Raymond Kaminyoge na Elizabeth Edward mwananchipapers@ mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wamiliki wengi wa blogu katika mitandao ya kijamii nchini wamesema “kwaheri ya kuonana”.
Wamewaaga watumiaji wa blogu hizo ambao walizoea kupata taarifa muhimu za Serikali na matukio mengine ya kijamii kwenye kurasa zao za mitandao ya intaneti.
Sasa hawawezi tena kutuma taarifa hizo kwa kuwa kwanza watatakiwa kulipa Sh100,000, halafu ada ya Sh1 milioni kwa ajili ya kupata leseni na pia uwezekano wa kudhibitiwa baada ya kusajiliwa.“Gharama kubwa za usajili wa leseni zimetushinda. Tunasitisha huduma kwa muda usiojulikana,” alisema mmiliki wa blogu ya Innowisetz, Innocent Shayo kupitia mtandao.
Baadaye akizungumza na Mwananchi kwa simu, Shayo alisema gharama za kupata leseni ambayo ni Sh1 milioni ni kubwa hasa kwa blogu ambazo zimeanzishwa hivi karibuni.
“Serikali ipunguze ili ziweze kulipika kwa urahisi,” alisema.
Shayo alitumia ukurasa wake kuwaaga wasomaji wake akisema hakupenda kusitisha huduma, lakini ameamua kutii agizo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Shayo ni mmoja wa wamiliki kadhaa wa blogu waliotuma taarifa kwenye mitandao ya kijamii wakisema wanasitisha huduma kwa sababu wameshindwa kulipa gharama za usajili wa leseni. TCRA iliagiza kuwa ifikapo Juni 15 (yaani jana) vyombo vya habari vya maudhui ya mtandao ambavyo havijapata leseni havitaruhusiwa kuweka taarifa au habari zozote kwenye akaunti au kurasa zao. Sharti la usajili wa majukwaa hayo ya mitandaoni ni kwa mujibu wa Kanuni za Maudhui ya Kimtandao zinazolenga kuratibu na kudhibiti matumizi sahihi ya mitandao. Kwa mujibu wa kanuni ya 4 na 14, watu wanaotoa huduma za blogu, majukwaa ya mtandaoni wanatakiwa kujisajiliwa na chombo hicho.
Katika awamu ya kwanza Mei 25, mamlaka hiyo ilitoa leseni 45 kati ya 262 kwa watoa huduma hizo.

Umoja wa Wamiliki wa Blogu Tanzania (TBN) una wanachama 130, lakini waliosajiliwa ni watano.
Mtandao maarufu wa Jamii Forums ulikuwa wa kwanza kuwaaga wasomaji wao kwa kuwaomba radhi kwa usumbufu. “Kutokana na notisi iliyotolewa na TCRA Juni 2018 inayotutaka kusitisha utoaji wa huduma mara moja tunalazimika kutii agizo na tunasitisha,” ilisema taarifa ya mtandao huo.
Mmiliki wa blogu ya Darmpya.com, John Marwa aliungana na wenzake kuwaaga wasomaji, akisema kilichowashinda ni gharama za leseni.
“Tunasitisha huduma ili kuepuka kukwaruzana na TCRA. Masharti yaliyopo kwa sasa hatuwezi kuyatimiza,” alisema. Marwa alisema wataendelea kuiomba Serikali kufikiria upya gharama za kupata leseni ambazo alidai kuwa wengi hawawezi kuzimudu.
Mitandao mingine iliyowaaga wasomaji wake jana kupitia kurasa zao ni pamoja na Blogu ya Habari, mtandao wa Makonda Media na Bongo News.
[COLOR=rgb(184, 49, 47)]Hata hivyo muda mfupi baada ya TCRA kuanza utekelezaji wa kanuni za maudhui, wamiliki wa blogu na mitandao ya habari wamenza kutofautiana.

Tofauti hiyo imekuja baada ya baadhi kujisajili na wengine kupinga kwa madai kuwa kanuni zilizopo zinaminya uhuru wa habari.
Mkurugenzi wa Jamii Media inayomiliki mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo alidai kanuni zinalenga kukandamiza uhuru wa utoaji na upataji wa taarifa.
“Watu wanaweza kuona hili jambo ni la mchezo. Kwa kanuni hizi, kwenda kusajili ni kujitia kwenye kitanzi. Tatizo jingine ni kwamba Watanzania hatuna uelewa wa sheria,” alisema.
Melo alisema yapo mambo mengi kwenye kanuni hizo ambayo yanatishia haki ya kupata habari, akitoa mfano wa maelekezo ya kuweka wazi chanzo cha taarifa iliyotolewa.
“Hii ni zaidi ya kusajili na kupata leseni na wapo wanaofikiri inamhusu mtu au blogu fulani, hapana. Hili ni la kila mtu anayetumia simu au kompyuta,” alisema. Wakati huohuo, TCRA imeongeza muda wa usajili wa watoa huduma za maudhui mitandaoni hadi Juni 30, mwaka huu.[/FONT]
[FONT=times new roman]Awali, siku ya mwisho ya kujisajili ilikuwa Juni 15. Taarifa iliyotolewa jana jioni na mkurugenzi mkuu wa TCRA, James Kilaba ilisema wale ambao hawajajisajili wanatakiwa kufanya hivyo kabla ya Juni 30.[/FONT]

Mambo magumu daah kama jela vile

Ni jela Ntolilo maana uhuru wa kupashana habari hakuna tena. Wakati mtandao umerahisisha sana upashanaji wa habari duniani, hawa wameamua kuturudisha nyuma ili kumfurahisha dikteta mwenye kuihofia sana mitandao nchini.

Asiekubali kukosolewa ni mpumbavu wazuie na whatapp nayo basi ili tubaki na tbc kama mpasha habari.

Lee Kuan Yew wa Tanzania

Kubuni vyanzo vya mapato hawajui kazi kukimbizana na viada vya leseni kweli hawana plan

Shida iliyopo hapa wala hata siyo hizo leseni au usajili…

Kuna watu wanatafutwa hapa… yani wakiongea tu watakiona cha mtema kuni, wakipost tu wataivishwa kama mahindi…

Wale wanaoikosoa, kuielekeza, kuishauri na hata kuiambia serikali nini cha kufanya hao ndiyo target…

Cc: @Mahondaw

Kagame wakati mwingine anamdanganya tu huyu jamaa.

hili swala la kulipia blogger na youtube bado haliingii hakilini kabisa mamae. Waliotengeneza hizo platforms mbona hawajaweka vigezo vya kisenge kama hivyo? lengo lao ni kwamba habari imfikie mtu haraka iwezekanavyo popote alipo no matter iwe fake au OG wewe msomaji ndo utachambua na kuujua ukweli.

Daaaaah kweli tumefika hapa

Daah!! Inatia hasira sana

[MEDIA=twitter]1008099644356939778[/MEDIA]

hii hali mbaya sana sijui tutapita vipi kwenye hili janga

Bado natafakuri nyingi akilini mwangu,…kuna wakati unatamani hata kuongozwa na “kipofu”

Ni hivi hata wao CCM mapambio yao watashindwa namna ya kuyafikisha.

Asilimia kubwa, JF ilitumika sana kuijenga CCM bila wao kujuwa.
Sasa kuiminyaJF kuna hasara kubwa kwa CCM kuliko upinzani

Wasomi wa Tanzania ni wachumia tumbo Check Engineer James Kilaba anavyoaibika kama Jaji [B]MITUNGI/B yaani wanaweka usomi wao pembeni kisa njaa tu.

Hali si nzuri kwakweli,watu hawapendi kukosolewa.
Changamoto ni kuzitatua na si kuzikimbia.

Wakimaliza huko wataenda kwenye mitandao ya simu kupandisha gharama za data hili wananchi wengi washindwe kumudu gharama za matumizi ya internet.

Ngoja ifike 2020 tutaona