WALE WATENGENEZAJI WA BOMBADYEE CANADA, TUNAZUIA VINAVYOHAMASISHWA KAZI IPO.

Canada imepitisha sheria rasmi kwa nchi nzima inayoruhusu matumizi ya bangi.

Sheria hiyo hatimaye ilishinda kwa kupata kura za ndiyo 52 zinazoruhusu matumizi ya bangi hadharani,huku kura 29 za maseneta zikisema hapana.
Kutokana na kupitishwa kwa sharia hiyo sasa itawachukua majimbo,Manispaa na mamlaka takribani wiki kati ya nane hadi 12 kutengeneza masoko mapya ya kuuza bangi.

Lakini pia muda huu kabla ya kuanza kutumika kwa bangi rasmi,utatumika na Polisi kuandaa mifumo mipya ya kisheria.

Kwa mjibu wa sheria hii mpya mtu ataruhusiwa kuagiza bidhaa hii ya bangi kwa mfumo wa kimtandao kutoka kwa wasambazaji wanaotambulika kisheria.
[ATTACH=full]177819[/ATTACH]

source :bbc

wasisafiri nayo huku.

sidhani kama utafiti ulishawahi kufanyika bongo ili kupima madhara ya bange ukilinganisha na vilevi vingine kama pombe na sigara, pia kujua matokeo ya matumizi ya madawa mengine ya kulevya kama cocaine na heroine kama bange ikiruhusiwa. Tumeipiga marufuku kwakua tu mkoloni wetu aliipiga marufuku, ni wakati sasa umefika bange itendewe haki isiitwe “madawa ya kulevya” bange ni mmea tu na haitengenezwi maabara kama cocaine au panadol. vijana wataacha kujidunga ma heroine na ma cocaine watavuta bange kistaarabu, pia kuna soko zuri la bange linachipuka kwa kasi huko ulaya na america

NINGEKUWA RAIS NINGEWAULIZA WANATAKA GUNIA NGAPI WANIPE BOMBADIA 5 ZA BOENG 777:D:D:D:D:D:D

Imekaa safi sana hii, hongera Canada

Kenya naona nao wanataka kupitisha…“how comes mmea wa mungu upigwe marufuku kutumika”…ndo venye wakenya wanasema

Bombadia za boeng?