Vipi Kuondosha Wasiwasi Wa Mashaka Ya Najsi

#1
SWALI: Asalam alaikum ndugu waislamu Mbele yayote naomba Mola abariki kazi munazozifanya na awalipeni. Mimi ninatatizo ambalo linanisumbua mpaka wakati mwengine huwa nasikia kama kichwa kinanizunguuka, na tatizo hili nilamashaka,yaani naweza nikatoka chooni nikiwa nilisha jisafisha,ama nikamaliza kutawaza kabla yakusali lakini bado nikawa na mashaka kwamba kuna maali ambapo bado kuna uchafu ama hapakufika maji,na hizo mashaka zinanisumbua mpaka nakosa amani, vile vile wakati wakujitwaharisha.katika hali kama hiyi sijuwi niwe nafanya nini? Pia watoto wangu wanaweza kunya ama kukojowa mkojo ukaruka maali pengi ambapo sioni maali pengine ambapo ule mkojo umerukia, naweza nikawabadili nepi na nikawafuta lakini bado nikawa namashaka kuwa kunamaali pengine ambapo bado kuna ile najisi katika maali ambapo ule mkojo ulirukia ama mavi hata kama siioni(mkojo au mavi) ila nahisi tu kama kunamaali ambapo bado kuna najisi ila sijuwi ni wapi ,nakama nichumbani njo walirushia mkojo ama mavi,huwa nakuwa na wasiwasi kwamba kuna maali ambapo bado kuna najisi hata kama sioni iyo maali ,nini chakufanya ikitokea hali kama hiyo? Nikisualia iyo maali ama nguo ambazo nilikuwa navaa ule wakati na ambazo pia nina wasiwasi nazo sala inakubaliwa ama haikubaliwi?
photo_2020-02-20_21-35-24.jpg jibu:
 

danjones

Village Elder
#2
Asalaam aleikum! Usiwe na wasiwasi baada ya kutawaza kwa sababu ya kusali. Ukishamaliza kutawaza, endela na sala. Mungu mwenye enzi ni mwingi wa rehema. Kadhalika Mungu muumba vyote si mateka wa maisha wa binadam. Mungu anatuelewa vyema. Anelewa nguvu zetu zote na udhaifu wetu wote. Udhaifu wetu hauwezi kumzuia Mungu mwenya rehema kusikia na kupokea maombi yetu. Kwa hiyo, tawaza na kisha endelea na sala. Natumai jibu hili linakusaidia kiasi na swali lako. Mungu akurehemu wewe mtumishi wake.
 

Top