Ushenzi wa Mwafrika Inahitaji Tiba Ya U shetani?

Mungu ameshindwa! Basi mbona mwafa? Hata Askofu wa wakatoliki amekubali. M’protestanti wa kizungu amesalimu amri. Na wa Afrika wenye kufuata mienendo na dini za wazungu wamesalimu amri pia. Kifo kwao! Wanakufa na Covid-19. Jiulize, mbona " Bishop" Wanjiru ako na korona? Mbona wenzake Nigeria wamekufa?

Jawabu shwari! …Jitegemee! Miungu ya Afrika imewapa afya bora bila “mali”, ni mitishamba na ni migodi! Covid- organics, na vinginevyo. M’wafurushe hao wazungu warudi kwao na vigegezo vyao vya uboro!

Hamna haja ya masomo ambayo hayasaidii! Miaka zaidi ya 50, mwafrika amesomea Harvard, Oxford, na wakirudi kwao bado ni watumwa wa usomi! Itambidi mwafrika asizidi kupumpawazwa na masomo bure bure! Jiinue mwafrika! Hakuna mzungu huenda Afrika kumtajirisha Mwafrika. Wao huenda Afrika kwa anasa, kujipendekeza, kukidhi wizi wa rasilimali , ngono, na kwa U tumbili wa kizungu!