Ushauri wa hiari kwa wanajf academia wenzangu.

Ni dhahiri kwa sasa tuko ukimbizini na sababu ya kufika huku ni sisi wakosoaji kwani tungekuwa tunasifia haya yasingetokea. Hakuna shaka hili likikuwa jukwaa pendwa na bora la kiswahili na la nyumbani. Jukwaa hili limetuweka pamoja watu wa kada mbalimbali kuanzia wasomi wa kada mbalimbali, viongozi wadini na waumini wao, viongozi wa serekali na watumishi wao, viongozi wa siasa wote na wafuasi wao nk. Hivyo kukosekana kwa jukwaa hili huko nyumbani ni homa kwa watumiaji wake na ahueni kwa wote iliokuwa mwiba kwao na wanafahamika.

Ni vyema kwa sasa wakati jirani akiwa katupa hifadhi tukatumia nafasi na jukwaa hili kuendelea kusimamia hoja zetu za msingi ili tusiwape njia nyepesi wenye nia ovu na hili jukwaa kupata sababu nyepesi kwamba tunataka uhuru ili tutukane na wala hatuna hoja. Nimeona baadhi ya post humu ndani tuna furaha iliyopitiliza ya jukwaa letu kurudi japo uhamishoni tunaishia kuonyesha furaha yetu kwa kejeli na matusi zaidi. Tupige vijembe kadiri tunavyoweza kwabi vinakubalika, tuwazodoe watetezi wote watakapokuja huku uhamushoni, ila tusihame kwenye hoja zetu za msingi. Tusifurahi mpaka tukakosa hoja na majirani zetu wakaishia kutuona tuna hoja nyepesi na matusi zaidi, kwani hata viongozi wetu ni rahisi kufanya mawasiliano na mamlaka za huku kwamva ni vipi waruhusu jukwaa la wao kutukanwa.

Kuna hoja nyingi za msingi ambazo hata viongozi wanaosimamia sheria zenye nia ovu watakosa nguvu. Mfano jambo la bajeti, jana Zitto Kabwe amechambua bajet vizuri na kwa uwezo wake. Na sisi huku jukwaani tulipaswa kufanya hivyo. Hii sheria kandamizi ya mitandao tunapaswa kuipiga vita kwa nguvu zote. Jambo la katiba mpya pia ni vyema tukalijadili kwa nguvu zetu zote. Muelekeo wa uchumi wetu ulipo na mwelekeo wake ni upi chini ya awamu hii. Pia itapendeza sana tukianza kujadili nani anafaa kugombea urais 2020 kulingana na hali ilivyo. Tukijikita kwenye hoja za hivi na nyingine nzuri zaidi ya hivi tutakuwa na nguvu kama vilivyokuwa vikundi vikivyokuwa nchini mwetu wakati wa ukombozi kusini mwa nchi za Africa. Kinyume na hapo tutaonekana ni kundi la wahuni tunaotaka uwanja wa kutukana na kukejeli lakini hatuna hoja wala ajenda ya msingi. Ushauri huu sio wa lazima; iwapo ni sahihi tuufanyie kazi.

Una hoja za msingi, ni MUHIMU kuunganisha nguvu

Mkuu umeongea ukweli mtupu,tulizingatie hili…

Sawa kabisa nami nakuunga mkono. Matusi hayafai kabisa. hoja tu ndio zitawale katika forum hii mpya.

UNA HOJA ZA MSINGI,TATIZO NI VIONGOZI TULIO WANASHAWISHI WATU KUTUKANA.KAMA KIONGOZI MKUU UNAWAAMBIA WATU WANAWASHWA WASHWA,UNATEGEMEA NINI?

Mkuu huku kwenye siasa hukutakiwi matusi bali vijembe, japo matusi hayakwepeki. Ila kikubwa ni kutokuhama kwenye hoja za msingi maana tunazo nyingi. Matusi yawe kwa baadhi ya wachangiaji wanaotaka kuvuruga mjadala. Na sio kuanzisha thread inayopandisha watu hasira na kuishia kutukana. Katika mazingira haya hata kama ndani yake kuna hoja ya msingi, watu wanaichukulia kama genge la walevi wenye jeuri tu.

Wenye madaraka na mamlaka yao wanachochea kwa matusi a kuchokoza kwa kejeli ili kuwaondoa watu kwenye mada. Mimi sikubaliani na upuuzi huo wa kuchokozwa na kuchochewa, huwa najibu kwa hoja na nguvu na aina ile ile hata tusi. Tumewachekea nyani tunavuna mabua.

Tumefikia hatua ya kunyonga hotuba mbadala kwenye bunge kwa watu kuogopa kukosolewa? Ka si usenge ni nini?

Naunga mkono hoja

mwifa, kuna hoja ya msingi, lkn kama Jiwe mwenyewe anatoa matusi (mfano eti hela itatokea matundu yote…) huyo lazima ajibiwe, atukanwe maana ametukana na hatuna uwezo wa kumkalisha chini na kumkanya. Mtu anajiita jiwe, tufanyeje, tutamuita jiwe. Tutamlaani, kila mmoja kwa nguvu zake akemee. Nakubali tusikemee kwa matusi bali kuonyesha mapungufu yake.

Ni kweli mkuu maana inafikia muda unalazimika kutumia lugha kali, ila hata kama itatulazimu kutumia hizo lugha kali ila hoja ziwepo pale pale

exactly , tunajenga hoja zenye mashiko makubwa na kumkanya inapobidi

Tuko pamoja mkuu
Nalog off

Wakati mwingine matusi yanakuja Automatically , maana kuna member wamekuja hapa kutuongezea hasira hawa ni lumumba.

Uvumilivu huwa una kipimo.

Mkuu mwifa nadhani wewe umenipata. Mtu akikuingia kichwa kichwa tumia matusi ili akili imkae sawa hilo halikatazwi, tatizo ni pale tunapojikita kwenye matusi zaidi kisha tunaacha hoja za msingi. Tupige hoja za msingi, kisha mtu akiingia kuharibu mada ipate fresh. Na kiongozi yoyote atakayetoa lugha ya matusi naye ajibiwe kwa lugha hizo hizo kwani ndio anaweza kuzielewa.

Umesema vema sana senior villager @Tindo…kusimamia hoja zenye kuweka msukumo wa mabadiliko ya maswala ya msingi ni muhimu sana.

kuna SAA misulule inachefua inabidi utumie lugha kali

Naunga mkono hoja…Nadhani humu hawakosekani hata baadhi ya viongozi walioichoka Hali ya sasa watasaidia kutupa nondo

nami naunga mkono hoja yako mkuu

hakika ameongea jambo la busara sana

Naunga mkono hoja kwa asilimia mia