Upishi wa vitumbua

[ul]
[li]Unachukua mchele, kisha unauosha na kuuanika juani, ukishakauka unausaga[/li][li]Unachukua unga wa mchele unachanganya na wa sembe na wa ngano[/li][li]Unaukoroga pamoja huku ukiupika mpaka uive kabisa[/li][li]Unauacha upoe, kisha unaweka hamira chapa maandashi na ya chengachenga(kijiko kimoja cha chai) ili uumuke vyema. Unauacha uumuke kwa masaa 4 hadi 5[/li][li]Unaongezea yai moja kisha unakoroga vyema, unaongeza na sukari kiasi unakoroga vichanganyike vyema[/li][li]Baada ya hapo unaweka kikaangio motoni, unaweka mafuta kidogo kwenye kila tundu na kumimina ule mchanganyiko wako[/li][li]Kwa kutumia vifimbo vya mishkaki unageuza pale upande wa chini unapoanza kugeuka rangi na kuwa brauni na kukiondosha kinapokua kimeiva[/li][li]Kitumbua chako kitakua tayari kwa kuliwa[/li][/ul]
[ATTACH=full]178393[/ATTACH]

Hakika mambo ni mazuri

Napenda vitumbua vya mayai sana

Aah…aaaaaah! nilidhani kupika papuchi.

Hiyo process ya pili niliwahi kuingia jiko moja nikakuta wanafanya huo mchanganyiko,nikajua wanafanya hivyo ili kujiongezea faida kumbe ndio utaratibu ulivyo…!!

Vinakuwa laini ndani

Hivi ni lazima vitumbua viwe vya round ?

sio lazima mimi huwa napikia kwenye kikaangio cha chapati