Jana asubuhi watumishi wa wizara ya uvuvi waliingia kwenye mgahawa wa Bunge bila kupata kibali toka kwa Katibu wa Binge, wala Spika wa Bunge, wala Naibu Spika na kuanza kupima samaki kwa “rula” ambao walikuwa wameshapikwa na tayari kuliwa!
Hivi sasa ndiyo Bunge nalo lijionee namna baadhi ya watumishi wa Umma namna wanavyotumia madaraka yao vibaya wakifuata nyayo za kule juu kwa Jiwe!
Vile vile kwa kuwa wizara hiyo inaongozwa na swaiba wake Magufuli, Bwana Mpina, basi tujue kuwa jambo hilo litazimwa kimya kimya…
Naanza kuyakumbuka maneno aliyotamka Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, wakati ule kuwa utawala wa huyu Jiwe hautamuacha hata mtu mmoja salama…
Ameanza na sisi wapinzani kutunyamazisha na baadaye atakuja kwenu…
Sasa ndiyo hiki kinachotokea kwa watumishi wa wizara ya Uvuvi kujitwalia ujasiri usio wa kawaida na kwenda na “rula” zao na kuanza kuwapima samaki hao!
Hili Taifa, tupende tusipende linaelekea kuangamia, kutokana na kiburi cha mtu mmoja aitwae Magufuli!
Kwa kuwa katika mazingira ya nchi inayofuata utawala bora unaozingatia sheria, kwa kitendo cha hovyo kabisa kilichofanywa na watumishi wa wizara ya Uvuvi, ilibidi barua ya kujiuzulu iwe ishamfikia mteule wake Rais asubuhi hii
Magufuli hana ubunifu wowote zaidi ya kuua watu wenye maono yaliyomzidi mawaziri wake kama akina mwigulu hata pm hawataweza isaidia nchi .jiwe anategemea maboya kama akina bashite hawezifanikiwa ataondoka madarakani kwa aibu sana muda unazungumza
umefuata nini huku wewe uvccm? wakati jiwe anaanza kudhibiti mitandao mlikuwa manashangilia, mlidhani nyie mtaruhusiwa hamkujua bila sisi wapinzani nyie mamwezi kupata credit
Jambo baya sana kitu kipo tayari kwa kuliwa wewe unakuja mikono yako na mirula sijui ya wapi unaanza kupima sio vizuri kwa afya.
Vip hao samaki waliendelea kutumika au walitupwa
yule boya aliyekua anapima samaki alitegemea igizo lake kushangiliwa na mitandao na vyombo vingine vya habari bila shaka, lakini matokeo yake anaonekana kama taahira tu anayelipwa mshahara wa utumishi bure