Ujuzi wa kutengeneza maziwa ya mtindi

Nina lita 5 za maziwa fresh nimeletewa na jamaa yangu,mimi kwa ujumla maziwa fresh siyafagilii sana,naomba mwenye ujuzi anielekeze ninafanyaje haya maziwa ili yaweze kuwa mtindi maana hata familia yangu wote nao ni wapenzi sana wa maziwa mtindi…

Chemsha maziwa kwanza alafu ngoja yapoe. Changanya maziwa haya na kikombe nusu hivi cha maziwa mtindi. Ngoja mda wa siku mbili au tatu yatakuwa tiyari.

Kumbe ni lazima niwe na maziwa mengine ya mtindi,kwahiyo kama sina,haya niliokuwa nayo hayawezi kuwa mtindi yenyewe…?

Hii ndio njia ya uhakika ninayoifahamu. Yaweza pia yakawa mtindi yenyewe lakini huenda matokeo yakawa tofauti kulingana na usafi wa vyombo unavyotumia.

Hufagilii Fresh? Unataka mpaka yachache…

Ukichemsha maziwa hakuna mtindi hapo. Yaache hivyo hivyo bila kuyaweka kwenye friji wala kuyachemsha yatakua mtindi ndani ya siku mbili au tatu

Yaache tu kny huo mtungi kwa siku mbili hadi tatu kutegemea na hali ya hewa …kama kuna joto yatageuka mtindi haraka ila kama kuna baridi yataweza kwenda hadi siku nne.

Weka sukari yata oza haraka ndio maana ya maziwa mtindi yaliyooza huita maziwa Mara, au lala

Huwa nashindwa kuelewa rafiki mie nilikuwa najua ka wewe kwamba mtindi ni maziwa fresh yanaekwa mpaka yachache sasa nikaja sikia eti mtindi huu wa kupima huwa ni maziwa fresh yanachemshwa ndipo yanawekwa na kuja kuwa mtindi sio siri nilishangaa sana.

Ila wanaofahamu watuambie unachemshwa ili uweje sababu huo unaochemshwa unakuwaga na harufu ambayo sio nzuri kabisa.

Ndio nimeona leo maajabu haya

Limao inaweza tatua tatizo, wenye uzoefu waje

Nipe maujuzi pls @Ukhuty

Ipo kitambo ila sijawahi waelewa wana maana gani

Taaluma yangu hii.

Maziwa tunachemsha ili kuua bakteria na vijidudu vingine. Bakteria waliopo kwenye maziwa yaliotoka kwa Ng’ombe yanakuwa contaminated na chombo, mikono, hewa, chuchu nk.

Bakteria hawa wapo wanao gandisha na wapo ambao huya haribu au kuozesha.

Sasa tunachemsha (pasteurization) ili kuua bakteria wote. Tukisha yachemsha ndipo tunaweza amua tutengeneze Mtindi au Yoghurt.

Kama ni mtindi, una yapooza mpk joto la 25C, na kuweka starter culture au mtindi kidogo ambao ulisha ganda na unauacha kwa siku nzima au 18hrs. Na Yoghurt ni hivyohivyo sema utofauti ni temperatures ya incubation ni 43C kwa saa 4 Yoghurt inakuwa tayari ishaganda inabidi uweke kwenye friji ktk ubaridi wa 4C kwa saa 8 for aging.

hahaah usijali nitakupa ya kutosha

nakumbuka kuna siku nilishawah kunywa jag zima la maziwa ya mtindi uliochanganywa na uji nikawa nashushia kwa mkate na samaki, baada ya gesi kuishia njia, kesho yake nilishnda karb na mlango wa choo karb nusu siku, sikutaka kujua nini kilisababisha ila tangu siku ile sitak mtind tena. Nakumbuka kazn niliwaambia nimepata msiba.

Ila mazuri sana kama unakunywa glasi moja kila siku,ubaya ukinywa mengi lazima utaendesha…

Nackilizia madini ktk hii thread.

[ATTACH=full]176740[/ATTACH]Asanteni wadau nimefanikiwa kutengeneza mtindi wangu mwenywe nyumbani,ingawa sikutumia ile njia ya kuwa na stater ya mtindi ,niliyalaza kwa siku moja kufika asubuhi it’s done …