UJERUMANI NI MBABE,JEURI,MBISHI ASIYESHINDWA KIRAHISI MKOROFI LAKINI MZALENDO.

ze-dudu

Senior Villager
#1
Tarehe kama ya leo miaka 104 iliyopita (Tarehe 28 June mwaka 1914) Archduke Franz Ferdinand wa Austria, aliuawa katika mji wa Sarajevo huko Serbia na askari wa Yugoslavia. Mauaji haya yalisababisha mgogoro mkubwa wa kidiplomasia kati ya Austria-Hungary na Serbia. Tarehe 28 July mwaka huohuo, Austria-Hungary (swahiba wa karibu wa Ujerumani) akatangaza vita na Serbia kufuatia mauaji hayo. Urusi akaingilia vita hii na kuanza kumobilize jeshi lake ili akaisaidie Serbia ambayo ilikuwa inakaribia kushindwa.
Ujerumani akatoa "ultimutum" kwa Urusi kumtaka aache kuingilia vita hiyo na aamue kudemobilize jeshi lake, vinginevyo atampiga. Urusi akakaidi agizo hilo la Ujerumani na kuendelea na mpango wake wa kumobilize jeshi lake ili kuisaidia Serbia. Kutokana na ukaidi huo wa Urusi, ilipofika August 1 mwaka huo Ujerumani alitangaza vita na Urusi. Akamvamia na kumtandika.
Maji yalipozidi unga, Urusi akaomba msaada kwa maswahiba zake wa Tripple Entente (Ufaransa kwa upande wa Magharibi na Japan kwa upande wa mashariki). Mwezi August Ufaransa akaanza kumobilize jeshi lake ili amsaidie Urusi kwa kuipiga Ujerumani kutokea magharibi. Ujerumani kuona hivyo tarehe 3 August akatangaza vita na Ufaransa. Akamvamia na kumtandika.
Mpaka kati ya Ujerumani na Ufaransa ulielemewa majeshi. Ubelgiji ambayo ni kiunganishi kati ya Ujerumani na Ufaransa upande wa kaskazini mashariki ilikuwa eneo muhimu la vita. Ujerumani akaipa option Ubelgiji ichague upande. Either iungane na Ujerumani ambaye ni jirani yake upande wa mashariki au iungane na Ufaransa ambaye ni jirani yake upande wa kusini. Ubelgiji na Laxembourg zikachagua kuwa neutral, yani kutokuwa na upande. Ujerumani akadoubt neutrality yao. Akazivamia na kuzitandika.
Akaingia Ubelgiji na kupata fursa ya kuipiga Ufaransa kutokea Kaskazini. Uingereza akakerwa na hatua ya Ujerumani kuipiga Ubelgiji ambayo ilikuwa neutral. Tarehe 4 August Uingereza akatangaza vita na Ujerumani.
Upande wa mashariki Urusi na washirika wake walikuwa wakipigana vikali na Austria-Hungary swahiba wa Ujerumani. November mwaka 1914 Ottoman Empire (Uturuki ya leo) ilijiunga na Central power (kundi la Ujerumani na Austria-Hungary) na kusaidia upande wa mashariki na kuasisi vita maeneo ya Mesopotania na Penisula ya Sinai.
Mwaka 1915 katikati ya mapigano makali Italy na Romania zkaungana na Triplle Entente (kundi la Uingereza na washirika wake), na Bulgaria akaungana na Central power (kundi la Ujerumani na washirika wake).
Mwaka 1917 Ujerumani ilizamisha meli 7 za mizigo za Marekani, katika kile kilichoelezwa kuwa mpango wa Ujerumani kuitandika Marekani kwa kupitia Mexico. Kufuatia meli zake kuzamishwa, na hofu ya kuvamiwa, Marekani akaamua kuchagua upande haraka. Akaungana na Waingereza, na akatangza vita na Ujerumani tarehe 6 April mwaka 1917.
Wakati Marekani anajoin vita hiyo, Urusi alikuwa ameshaanza kuzidiwa, kutokana na kipigo kikali cha Ujerumani na washirika wake. Kipigo hicho kilisababisha serikali ya Urusi kuvunjika vipande vipande kufuatia mapinduzi ya February na October mwaka huo. Hatimaye Urusi akasurrender na kuomba maridhiano kupitia mkataba uliojulikana kama "Treaty of Brest-Litovsk." Huu ulikuwa ushindi mkubwa kwa Ujerumani na washirika wake (Austria-Hungary, Uturuki na Bulgaria).
Kwahiyo upande wa mashariki vita ikaisha kwa Urusi ku-concide defeat. Lakini upande wa magharibi vita ilipamba moto. Kati ya mwaka 1915 hadi 1918 Romania, Ureno, Hejaz (Saudi Arabia), China, Ugiriki, Thailand, Albania, Montenegro, Laxembourg, Brazil na Armenia zilijiunga na Tripple Entente kwa nyakati tofauti na kuongeza nguvu kwa kundi hilo. Hii ilifanya Ujerumani kuanza kurudi nyuma upande wa magharibi.
Tarehe 4 November mwaka 1918 Austria-Hungary iliconcide defeat na ikasaini mkataba wa kusitisha vita uliojulikana kama Armistice of Villa Giusti. Baada ya swahiba wake kussurender, Ujerumani nae akakubali yaishe tarehe 18 November mwaka 1918, na hivyo kufanya vita kuu ya kwanza ya dunia kumalizika.
Ukiondoa nchi makoloni ambazo zilipigana upande wa watawala wao (colonial master), nchi huru zilizoshiriki vita hiyo zilikuwa 26. Kundi la Ujerumani (Central power) lilikuwa na Pioneers wanne tu wa vita hiyo (ukiondoa client states na Co-belligerent states). Kundi la Uingereza (Tripple Entente) lilikuwa na nchi 22 zilizoshiriki moja kwa moja vita hiyo.
Ni sawa na kusema kuwa nchi 4 zilipigana na nchi 22, ambao ni wastani wa nchi 6 kwa nchi moja. Kwa lugha rahisi ni kusema kwamba nchi moja katika kundi la Ujerumani ilipigana na nchi 6 kwenye kundi la Uingereza na washirika wake. U can see how powerful Germans na washirika wake walivyokuwa. Muungano wa maifa 23 kupigana na Ujerumani na washirika wake ni kielelezo kuwa Ujerumani ni taifa la kibabe na linaloogopwa.
Uingereza na washirika wake 22 (Tripple Entente) ni kusanyiko la waoga (the united of cowards). Hii ndio sababu nchi nyingi za Ulaya hadi sasa hazimkubali sana Mjerumani kwa sababu zinamuogopa. Kwa kifupi Ujerumani hajawahi kupendwa na watu waoga. Ujerumani ni mbabe, jeuri, mbishi, asiyeshindwa kirahisi, mpambanaji, mkorofi lakini mzalendo. Yupo tayari kufanya lolote kwa ajili ya taifa lake.
C&P
1530307387643.png
 
#2
Hawa wajerumani ni watu makini sana na ni wenye akili sana.
Baada ya vita hivi vya kwanza kuisha kwa ujerumani kushindwa vita na kusalenda, waingereza, wafaransa na washirika wao walimnyang'anya ujerumani makoloni yote ikiwemo Tanganyika na kumbana sana kiuchumi (kwa kumtoza faini kubwa na kumlazimisha apunguze majeshi na manoari za kivita) na baadae kudhohofishwa zaidi baada ya vita vya pili vya dunia. Ila hawakukata tamaa wakaanza kuujenga uchumi wao mpaka sasa ni nchi ya kwanza kiuchumi barani ulaya ikifuatiwa na muingereza na ni ya 4 duniani chini ya USA, Uchina na Japani.
 

Top