Uhusiano wa mageuzi ya mifumo ya Kijasusi na uchumi wa nchi.

Mji wa Sevastopol nchini Urusi ulianzishwa tarehe 14 June 1783 miaka 235 sasa. Kila jasusi wa Urusi anapomaliza mafunzo yake kabla ya kuanza kazi rasmi hufunzwa kwa kutamka juu ya mji wa Sevastopol kwamba “Это место России в военную доблесть & славы, дорогие сердцам всех россиян” kwa lugha ya kitumwa (It is a place of Russia’s military valour & glory, dear to the hearts of all Russians)

Eneo hili ndio moyo wa taifa la Urusi katika kuiangaza Urusi pande zote za nchi hiyo, ndiomaana pengine ni sababu tosha ya kuwalisha maneno hayo watumishi wa kada ya ujasusi wa shirika la ujasusi la FSB. Nchi yoyote duniani lazima iwe na kitu kinaitwa pin point, na kwa Urusi tangu miaka 235 iliyopita, mji huo ndio pin point yao, achilia mbali miji yenye mapori maalumu ya mafunzo ya kijasusi ya Zabaikalsk- Manzhouli, pia muundo huu unaweka utaratibu wa kila wizara, shirika, taasisi nk ya serikali lazima iwe na person contact wa FSB, wao wanaita jasusi mwangalizi. Mfano katibu wa wizara ya kilimo akiwa na jambo haendi moja kwa moja kwa waziri wake, ni lazima awasiliane na mtu wa ujasusi wa ngazi inayolingana na yeye, pia waziri haendi moja kwa moja kwa rais mpaka kwanza ashauriwe na mtu wa ujasusi.

Muundo huu haupo mbali, nchini Tanzani wakati Tawi Maalumu (Special Branch SB) linaundwa baada ya uhuru na Mwalimu Nyerere hasa baada ya maasi ya 1964, mfumo ulibadilika kutoka ule wa Waingereza kwamba kila mkuu wa shirika/taasisi au wizara kuripoti kwa mkuu wa Nchi, na kuuweka uwe wa Kirusi ambapo kila wizara/shirika au taasisi ikawa na afisa usalama mwangalizi, leo mfumo unafanya kazi kwenye mashirika na taasisi tu, umeakisi mifumo ya FSB.

Lakini msingi wa pin point bado umesalia kuwa imara ambapo Zanzibar ni division no 1, na Dar ni 2, Tabora no 3 nk… Zanzibar ni eneo mtawalia la kimbinu kwa Tanzania, Ili uilinde Tanganyika pande zote ni lazima usimame Zanzibar, na Ili uilinde Urusi yote ni lazima usimame Sevastopol, .

Mageuzi aliyoyafanya Rais Boris mwaka 1994 yaliubadili mfumo wa ukusanyaji taarifu, jina la shirika na uendeshaji wa shirika la ujasusi la FSB ambalo awali liliitwa KGB, kutoka kuhami siasa za madaraka ya chama tawala na kwenda kwenye kuhami uchumi, na matokeo yake yake ni kuibuka kwa nguvu za kiuchumi za Urusi ya leo hasa katika bishara ya silaha duniani, vilevile uchumi na maisha ya warusi yalibadilika kutoka taifa la walevi wa kupindukia hadi yaifa la wachapakazi na wabunifu,

Mageuzi hayo yalifanywa wakati huo Vlamir Putin akiwa ndie kiongozi wa KGB na leo ndie rais wa Nchi, ni wazi kuwa Shirika hilo kongwe duniani liliacha mifumo ya kijamaa ambayo msingi wake ni kuhami serikali na chama kilichopo madarakani na kuelekeza nguvu zake katika kuhami uchumi na maslahi ya nchi wakijikita katika utafiti wa biashara na masoko huko somo linaloitwa Marketing Spy likipewa uzito mkubwa katika uwanja wa kijasusi.

Afrika imepambazuka, Kenya idara yao ya ujasusi wameifanyia marekebisho, Zambi pia, Botswana nao hawakukaa mbali, Ghana nao wamefanikiwa. Kwasehemu kubwa msingi wa mageuzi ya idara za ujasusi za nchi zote hizo ni kwamba mataifa ya afrika yamepitia na kufuzu hatua tatu za ukuaji, Kwanza ni kudai na kupata uhuru, pili ni kujitawala na kudumisha madaraka, na ya tatu sasa ni kujenga uchumi wa nchi zao. Katika hayo wanaamini sasa tunaweza kujitawala na hakuna tatizo kwa chama chochote tena kushika madaraka kwakuwa misingi yote ya nchi ikiwa ni katiba, bunge, mahakama na hasahasa idara za ujasusi vipo imara, si muda tena wakufikiri juu ya kudumisha madaraka, bali taifa likue kiuchumi kwa sera thabiti na hapa chama chochote kinaweza kushika madaraka ilimradi taasisi za kinchi huko chini zipo imara.

Dunia ya uchumi ni uwekezaji, sio uporaji, hakuna taifa linaloweza kuhubiri nchi ya viwanda bila uwekezaji, China ilidumu kwenye mfumo wake wa kijamaa kwa miaka mingi wakijiita wao wanao muundo wao wakujenga nchi ya viwanda, lakini hawakufanikiwa, mpaka walipofunguamilango na kuweka sera nzuri za sifa ya kimataifa ndipo wawekezaji toka Marekani, Uingereza na Urusi walipoingia na kujenga viwanda hivi tunavyoviita viwanda vya china leo.

Mageuzi ya China yanamkono wa dunia, hakuna anayehubiri mageuzi huku kajifungia milango, mtaishia kugombana na kuzodoana kila mnaposhindwa mipango yenu, mtanyoosheana vidole kwamba wewe ndio mchochezi mara unatumika na mabeberu, mara unaowaita mabeberu wakija kwako unawaita wawekezaji wazuri, yule nae atafurahi ukishindwa jambo, wakikukosoa unawaita wezi na maneno kadha wa kadha ya kuvurugana wenyewe, lakini tatizo ni lilelile mnataka mabadiliko ya mdomoni bila kufuata misingi ya mabadiliko hayo, msingi mkuu wa mabadiliko ya nchi yoyote duniani huanzia kwenye idara/shirika la ujasusi na Tanzania ni lazima kubadili mfumo mzima wa Idara ya usalama wa Taifa na vyombo vingine tanzu kama vile Jeshi la Polisi nk, mifumo iliyopo ya vyombo hivi haina uhusiano na uchumi hasa uchumi wa leo wenye vita vya kijasusi. Ni mfumo wa kisiasa na kiutawala zaidi.

Na Yericko Nyerere

[ATTACH=full]177162[/ATTACH]

Ni kweli wewe ni yule mzee wa mbutu kigamboni?kwani kwa sasa huku uhamishoni bwana kuna vibwengo vimejitokeza kuja na majina ya watu toka jf!!ila kwa andiko hilo sina shaka sana!!!

shukrani Mkuu,nikusumbue kidogo naomba nami nifundishe japo kiduchu ili nami nimfanyie ushushu jiwe kuu ili nijue kama anavinasaba vya kishetani au la!

Umekuja huku hahahaaaa

Kwa mara ya kwanza umeongea kijasusi kweli kweli!!

@Yericko Nyerete

Hili suala la kukosea kuandika “username” naona limewakumba wengi sana humu ndani.

Unaona kabisa huyu alikusudia kuandika jina fulani ila alikosea herufi.

mods @The Tweet ungetafuta namna ya kuwasaidia hawajamaa.

Karibu kaka yeriko

Karibu mkuu. Namsubiri Nguruvi3, Mukandala, Ruttashubanyuma etc hoja nzito ziendelee

Kumekucha

welcome Yerico. naona umeandika ukweli mtupu tena kwa uwazi zaidi, nchi yetu bado iko kwenye mfumo wa kizamani sana japo hawasemi lakini vyombo vya usalama vina mentality ya kulinda “chama na serikali” kitu ambacho ni kosa kubwa zama hizi. huwezi kua unapoteza resources za nchi kulinda “chama” wakati nchi imekomaa na ipo kwenye mfumo wa vyama vingi.

Naam

Nyerete?

Ame rekebisha tayari naona

Bikira

Karibu mkuu

Tatizo hao unaojaribu kuwaelezea sera nzuri, zilizo na umakini wanakuona mchochezi na unaingilia mambo yao…

Wao wakitaka iwe hivi basi iwe hivyi hivyo… iwe vibaya au vizuri usihoji…

Cc: @Mahondaw