Twaweza yamgusa dikteta sasa aamua kuwajia juu

BAK1

Village Elder
#1
TWAWEZA YATAKIWA KUJIELEZA KUFANYA UTAFITI BILA KIBALI

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Siku chache baada ya kutoa utafiti wake, Taasisi isiyo ya Serikali ya Twaweza imeandikiwa barua na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) ikitakiwa kujieleza ndani ya siku saba ni kwa nini isichukuliwe hatua za kisheria kwa kufanya na kutoa matokeo ya utafiti kuhusu maoni ya wananchi bila kibali.
Kwa mujibu wa barua hiyo inayodaiwa kuandikwa na Mkurugenzi wa Costech, Amos Nungu imesema Twaweza waliwasilisha maombi ya vibali vya kufanya utafiti wa awali nchini lakini utafiti huo wa Sauti ya Wananchi haukuwasilishwa katika maombi yao.
Soma zaidi… http://mtanzania.co.tz/wameporomoka/
“Matokeo ya utafiti huo yanakiuka kifungu cha 11 cha Mwongozo wa Kusajiliwa na Kuidhinishwa kwa Usajili wa Kitaifa kwa kutoandikisha mradi huu wa utafiti kwa Costech,” imesema sehemu ya barua hiyo.
Katika utafiti huo wa Twaweza, matokeo yalionyesha kuporomoka kwa umaarufu wa rais, vyama vya siasa, wabunge na madiwani.
 
Last edited:

BAK1

Village Elder
#4
By Tumaini Msowoya, Mwananchi tmsowoya@m,wananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imeitaka Taasisi ya Twaweza kujieleza ndani ya siku saba kwa nini isichukuliwe hatua za kisheria kwa kosa la kutoa matokeo ya utafiti bila ruhusa.
Barua hiyo ya Costech imesema, Twaweza waliomba kibali cha tafiti nne ambazo mmoja umekamilika na nyingine tatu bado zinaendelea.
Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosambaa mitandaoni ikionyesha imesainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Amos Nungu, tume hiyo ndiyo yenye mamlaka ya kusajili na kutoa kibali cha tafiti zote za muda mfupi na mrefu zinazofanywa nchini.
Barua hiyo imedai kuwa mwishoni mwa wiki, kulikuwa na taarifa za Twaweza kutoa utafiti uliopewa jina la ‘Sauti za Wananchi’ ambao, tume haina rekodi zilizoruhusu kuchapishwa kinyume cha sheria.


Soma Zaidi:
Ripoti ya Twaweza ilivyozua mjadala, sababu za viongozi kupoteza umaarufu
VIDEO:Ushauri wa Ulimwengu na maswali kuhusu utafiti wa Twaweza
“Kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 7 cha mwaka 1986, tume hiyo ndiyo yenye mamlaka kusajili na kutoa kibali cha kufanyika tafiti nchini,” imesema barua hiyo.
Taarifa kutoka Twaweza zinathibitisha taasisi hiyo kupokea barua kutoka Costech na kwamba wanaifanyia kazi.
Hivi karibuni Twaweza walitoa ripoti ya utafiti wa ‘Sauti za Wananchi’ ukielezea maoni ya wananchi kuhusu siasa nchini.
Utafiti huo umeonyesha kuporomoka kwa ukaribu wa wananchi na vyama vya siasa, utekelezaji wa majukumu kwa viongozi walioko madarakani, Rais anavyotekeleza majukumu yake tangu alipoingia madarakani na uhuru wa kujieleza katika baadhi ya maeneo.
 

Kylie

Senior Villager
#13
Mie hata sielewi Mkuu. Hivi alidhani nini alipoamua kugombea Urais!? Alidhani kuongoza nchi ni lelemama!? Afanye madudu yake chungu nzima kila kukicha huku Watanzania tukimuangalia tu huku tukiwa kimya na umaarufu wake bado uko juu!?

Ana akili finyu sana huyu
sio akili finyu mkuu, huyu ni Kichaa
 
#14
Dikteta katika ubora wake mkuu!! Ni wa kutisha kila taasisi amekamata!! wote wanatakiwa kumuimbia mapambia! kama yule Bibi yake pale JNIA alipomuita Nabii!! Tumekwisha!! jinamizi linatumaliza
 
#19
Tetesi za chini ya Kapeti ni kwamba TWAWEZA tu baada ya kutoa Ile report ya utafiti walishaitwa kujieleza Ikulu..
Yani huyu KICHAA anaimaliza Nchi..
Worse enough waliomzunguka bado hawajagundua huyu mtu kama ni Kichaa.
 

Top