Tuna Rais wa ajabu Tanzania ambaye hajawahi kutokea!

Hiyo heading ya topic yangu nimenukuu toka kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Mheshimiwa Tundu Lissu, ambaye hivi sasa yupo nchini Ubelgiji, kutokana na kupigwa risasi zaidi ya 30 na vyombo vya dola nchini

Ni ukweli usiopingika kuwa Rais Magufuli ni Rais wa ajabu ambaye hajawahi kutokea Tanzania tokea nchi yetu ipate Uhuru toka kwa mkoloni mwaka 1961, kama aalivyowahi kusema Mbunge huyo Tundu Lissu

Yeye tokea aingie madarakani amekuwa na kazi moja tu ya kupambana na yeyote ambaye anaikosoa serikali yake kuwa haifanyi vizuri katika uendeshaji wake

Amekuwa ni mtu ambaye badala ya kustawisha utawala wa kidemokrasia yeye ameirudisha nyuma nchi hii kwa upande wa demokrasia kwa zaidi ya miaka 50!

Kilele cha utawala wake wa mabavu ni kutufungia mtandao wetu pendwa nchini Tanzania wa Jamii Forum, hadi kusababasha tuwe “wakimbizi” kwenye nchi jirani kwa hii Kenyatalk

Huyu Rais badala ya kukubali kukosolewa ili ajisahihishe pale anapokosoa, badala yake anatumia vyombo vyake vya dola kumnyamazisha yeyote anayeikosoa serikali yake!

Hakika hawa CCM wametuingiza mkenge kwa kutuchagulia mtu ambaye badala ya kuliunganisha Taifa la Tanzania, yeye badala yake amaligawa na kuwafanya wapinzani wa nchi hii waonekane kama wahaini ndani ya nchi yao!

Ambacho anafanya Rais huyu ni kuisigina Katiba ya Jamhuri ya Tanzania ya mwaka 1977, iliyifanyiwa marekebisho mwaka 2005, Ibara ya 18(1) ambayo yeye mwenyewe aliapa kuitiii kabla hajaingia madarakani ambayo inaeleza wazi kuwa “kila raia wa Tanzania atakuwa huru kutoa maoni yake nje na Uhuru huo hautaingiliwa na chombo kingine chochote” mwisho wa kunukuu

Kwa mwenendo huu nchi yetu isahau kabisa kuwa na chaguzi zilizo huru mwaka 2020 na badala yake atapandikiza wabunge wake katika chaguzi hizo kwa msaada wa Jeshi letu la Polisi na Tume yake ambayo haiko huru ambayo wajumbe wake anawachagua yeye mwenyewe kuanzia Mwenyekiti wa Tume hiyo na wajumbe wake wote!

Mungu ibariki Tanzania

Kwani kuna nini?

Time will tell if its true…

tulichagua hovyo tujiandae kutawaliwa hovyo…

Mimi napita tu!

Kwanini wewe hujui??

Mtu mmoja anayejifanya yeye ni mungu mtu amefungia mitandao ikiwemo mtandao pendwa wa Jamii Forum, kisa yeye hataki kusemwa vibaya!!

Kama yeye hataki kusemwa vibaya atuachie urais wetu na yeye akaongoze familia yake ya mama Jesca

Hatukuchagua hivyo Bali Tume yao ya uchaguzi ndiyo iliyotuchagulia Rais tuliye naye sasa

Najurudia tena kusema kuwa tuna Rais ambaye hajawahi kutokea hapa Tanzania

Kwa kawaida mfumo wa vyama vingi maana yake wanasiasa mnajibizana kwenye majukwaa ya kisiasa…

Huyu Jiwe ameleta mfumo mpya wa siasa, ambapo mtu anayemkosoa yeye anaagiza vikosi vyake vya usalama “vim-shoot”

Si tumejionea kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu?

Yeye Rais alitamka hadharani kuwa mtu atakayepingana naye katika vita yake ya uchumi hawezi kusurvive!

Baada tu ya kutamka maneno yale tukashuhidia Mbunge wetu Tundu Lissu akimiminiwa risasi zaidi ya 30 tena mchana kweupe, tena kwenye makazi ya viongozi wa kitaifa…

Hivi sasa ni zaidi ya miezi 9 hakuna hata mtu mmoja aliyekamatwa na Polisi kwa ajili ya mahojia

Kila jiwe litageuzwa

Huyu si chaguo LA mungu

Yeye anachoamii ni hili cheo alichopewa hapa duniani cha Commander in Chief

Akiamini kuwa vile vifaru vya kijeshi vinavyomzunguka na yale magari ya Polisi ya washawasha, akiyaagiza wakati wowote kuwaangamoza wapinzani yatatii na kutekeleza maagizo ya Mkuu!

Tanzania inaongozwa na KICHAA hivihivi.

Mimi namulaumu Sana Kikwete Mrisho,ndiye alitusababishia Haya yote,ni sababu ya siasa za visasi kulipizana chuki na ubaguzi wa kikanda na kidini pia.

Magu dish lake limeyumba namna hii

https://www.youtube.com/watch?v=SJtl1QX_4eU

duuhh

Jenerali Ulimwengu alisema

Naunga mkono hoja

Yaaaani natamani nilie jamani. Oooooh Tanzania yangu.

Miguna nielekeze jinsi ya kuweka Avatar

Daah nimekua Miguna bila kupenda wallah…
Usijali juu kabisa kwenye dashbord hiyo ya notifications utaona wameandika K (K inawakilisha user name yako mi ilikuwaga M)[ATTACH=full]176300[/ATTACH] baada ya ku click hyo halaf edit avatar nishukuru badae