TUCHEKE, TUVUNJE MBAVU, TUONDOE STRESS

#32
Mlevi kakutwa akikojoa eneo la shule, Mwalimu mkuu akamuuliza, hilo bango hapo limeandikwaje?
Mlevi: 'USIKOJOE HAPA'.
Mwl: Kwahiyo unafanya nini hapo?
Mlevi kwa makini na upole akajibu: HAKI YA MUNGU NILIJUA NDIO JINA LA SHULE
 

stephot

Senior Villager
#34
*Ila jamani wanawake wa zamani walikuwa waelewa ,ebu chukulia mfano Yona alivyopotea zile siku ngapi halafu akarudi kwa mkewe akamwambia kwamba alimezwa na samaki na mkewe akakubali , ebu potea hata siku moja kwa mwanamke wa kisasa halafu mwambie hata ulimezwa na chatu uone kama atakuelewa!*
Atakuelewa tu,ila cha kushangaza lazima atakwambia mkapime Ukimwi,sasa sijui hapo vina uhusiano gani na kupotea kwako wakati ulishamwambia ulimezwa na chatu..
 
#39
Stress ni nini??
Stress ni pale umeenda kijijini kwa bibi ako huku umebeba jeans zako tano zile ja mtindo wa kuchanika (chanika jeans) sasa siku ukazifua ukazianika ukaenda zako kutembea ile unarudi jioni unakuta bibi yako kazianua afu kazishona zote
 
#40
Mwalimu kaniulizaa kama mtoto mdogo anaitwa mchanga... Je mtu mkubwa anaitwaje? ... Nikamjibu anaitwa kokoto..... Ameniitaa staff room labda atakuwa ameniitia chai

Huyu mwalimu ana roho nzuri sio kama mwl Msigwa.
 

Top