Sakata la korosho limefika patamu…
Ndivyo tunavyoweza kuita hilo sakata la korosho lilpofikia, ambalo wabunge wa mikoa ya Kusini, bila kujali itikadi zao za kisiasa, waliliongelea kwa uchungu sana, katika kikao cha Bunge kinachoendelea, ambapo baadhi yao walitokwa hadi na machozi!
Hapo Jana Chama cha Wanasheria nchini (TLS) kilitoa taarinyinginezo…ambia serikali hii ya awamu ya 5 kuwa ni makosa makubwa kuichukua pesa ya tozo ya kodi na kuifanya “yao”
Wakiendelea kueleza zaidi, Chama hiko cha Wanasheria, walisema kuwa tozo hiyo ya asilimia 65 inapaswa irejeshwe kwa wakulima na hiyo ipo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge hilo hilo ya mwaka 2010
Kwa hiyo Chama hiko cha Wanasheria nchini kimetishia kwenda mahakamani iwapo serikali itaendelea na azma yao ya kutaka kuwapora wakulima hao wa korosho hiyo pesa yao
Muungano wa vyama vya upinzani vyenye wabunge Bungeni nao umetoa taarifa yao ikielezea azma yao ya kutaka kulifikisha suala hilo mahakamani ambako wanaamini haki itapatikana
Nimekuwa nikijiuliza hili swali, hivi ni kwanini nchi hii inaingia kwenye migogoro na wananchi wake kila kukicha??
Ni dhahiri kuwa hivi sasa watawala walioko madarakani wameshaanza kulewa madaraka na wanafanya mambo ambayo hata hayamo hata kwenye Katiba ya nchi na sheria nyinginezo
Tunaendelea kukuomba ewe Mungu wetu tufanyie wepesi wa kuiondoa serikali hii madarakani ili kuliepusha Taifa hili lisiingie kwenye machafuko