Tetesi za soka 25 Juni

Kiungo wa kati wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 27, alitaka kuuziwa Real Madrid kabla ya fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kuchezwa mwezi Mei.

Babake ambaye pia ni mwakilishi wa mchezaji huyo Thierry Hazard anadaiwa kuwasiliana na Real Madrid kabla ya fainali hiyo mjini Kiev, Madrid akisema mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Hazard na Chelsea yamekwama hasa ikizingatiwa hawachezi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.

West Ham wako tayari kumpa kiungo wa kati wa England Jack Wilshere mkataba wa mwaka mmoja pekee kwa sababu wana wasiwasi kuhusu uwezo wake wa kukaa bila majeraha. Wilshere mkataba wake katika klabu ya Arsenal unamalizika majira haya ya joto.

Meneja mpya wa klabu ya Everton Marco Silva huenda akaamua kuwauza wachezaji nyota wa klabu hiyo ya Everton - wakiwemo kiungo wa Ufaransa Morgan Schneiderlin, 28, winga wa Congo Yannick Bolasie, 29, beki wa Wales Ashley Williams, 33, na mshambuliaji wa zamani wa England Wayne Rooney, 32.

Uhamisho uliopendekezwa wa Riyad Mahrez kutoka Leicester kwenda Manchester City unachelewa kwa sababu kiungo wa kati huyo wa Algeria mwenye miaka 27 anataka alipwe kitita kikubwa cha pesa na Leicester ndipo akubali kuondoka.

Mchezaji wa Ubeligji Marouane Fellaini, 30, amefichua kwamba utata kuhusu mkataba wake utatatuliwa hivi karibuni. Kiungo huyo wa kati wa Manchester United atakuwa bila mkataba hivi karibuni lakini amepokea ofa kutoka kwa klabu kadha.

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 25, amekiri kwamba alikuwa na “matatizo madogo” na meneja wa Manchester United Jose Mourinho msimu uliomalizika hivi majuzi.

Kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita, 23, anatarajiwa kurithi jezi nambari nane iliyokuwa ya Steven Gerrard katika klabu ya Liverpool.

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 30, huenda akatupwa nje ya kikosi cha kuanza mechi Argentina watakapojaribu kufufua matumaini ya kuendelea kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Nigeria Jumanne. Kocha wa Argentina Jorge Sampaoli inatarajiwa huenda akajiuzulu au afutwe kazi baada ya michuano hiyo.

Manchester United wako tayari kupambana na Manchester City na Real Madrid kumsajili mshambualiaji wa Ufaransa Kylian Mbappe 19, ambaye alikuwa akiichezea Paris St-Germain kwa mkopo kutoka Monaco.

Manchester United wanamuwinda beki wa kushoto wa Valencia na Uhispania Jose Luis Gaya, 23 baada ya dau la mchezaji waliokuwa wakimuwania Alex Sandro wa Juventus kuwa kubwa.

Manchester City imekuwa na makubaliano ya mdomo kuhusu kumsajili kiungo wa Napoli na timu ya taifa ya Italia, Jorginho, kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo.

Everton wanataka kumsajili mchezaji wa Chelsea, Ruben Loftus-Cheek, 22, na Jack Wilshere kutoka Arsenal.

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea ,Gunners, Olivier Giroud amesema kuwa kuondoka kwa Wilshere ni '‘pigo kubwa’'kwa Arsenal, akaongeza kuwa uamuzi wa kumuacha aende ni ''jukumu ‘’ la Meneja Unai Emery.

Nahodha wa Brazili, Thiago Silva, amemtetea mchezaji mwenzie Neymar kuhusu kitendo chake cha kulia uanjani baada ya kushinda mchezo dhidi ya Costa Rica kwenye michuno ya kombe la dunia. ‘‘Nilimwambia atoe yote aliyonayo moyoni, amekuwa akibeba mzigo mkubwa’’, alisema Silva.

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea ,Gunners

habari zote zina maana-ila hiyo ya mwisho ni habari ya kijinga

Huyu Hazard bench linamuhusu pale Bernabéu

Nadhani

kachamganya madesa

Ni zaidi ya ya Kijinga! Imekaa ki kunguru kunguru!