Tanzania Rasmi tumerudi chama kimoja

Sasa rasmi TZ tumerudi mfumo wa chama kimoja…ambapo kwa mara ya kwanza Bunge letu litakuwa ni la CCM kwa 100%. Halmashauri zote ( Local governments authority) zitakuwa chini ya CCM kwa 100%.

Huwezi kuamini lakini huu ndiyo ukweli …hii ndiyo TZ na hizi ndiyo siasa zetu kwamba tumerudi kinyumenyume kwa miaka 50.

Kwani imeandikwa wapi kwamba kuwa na chama kimoja ni vibaya

Sio vibaya kama kurudi huko ni kwa ridhaa ya wananchi walio wengi, na sio kwa madaraka ya urais yanayotumika vibaya. Mpaka sasa wapiga kura ni 1/3 ya wapiga kura wote waliopaswa kupiga kura. Ni ukweli usioacha shaka mwenendo wa chaguzi zetu toka Magufuli ameingia madarakani sio za ushawishi tena, bali ni kupitia matumizi mabaya ya vyombo vya dola. Chaguzi zote za marudio chini ya Magufuli tumeona ushenzi, ukatili na uhayawani wa wazi ili ccm watangazwe washindi. Uchaguzi wote wa serikali za mitaa ulinajisiwa mpaka haukufanyika kabisa, leo hii tuna viongozi mitaa wa ccm nchi nzima wasio na ridhaa ya umma, bali waliopatikana kwa maagizo ya rais aliye madarakani.

Kinachoendelea ndani ya nchi yetu sio ccm imara, bali ni kiburi cha madaraka cha rais wetu, ambaye anaitumia ccm kama kichaka cha kuficha matumizi yake mabaya ya madaraka. kabla ya uchaguzi huu ccm wameingia wakiwa na wabunge 28, na madiwani zaidi ya 1,000 waliopita bila kupingwa, na sababu ya kupita bila kupingwa ni kutokana na sheria zilizotungwa kwa nia ovu, na wapinzani kufanyiwa hujuma mbalimbali za kihalifu kama kutekwa, kuporwa fomu nk. Yote hayo tumeyaona kwa macho yetu. Kibaya zaidi uhalifu huu dhidi wapinzani unalindwa na vyombo vya dola, na sababu hasa ya vyombo vya dola kushiriki uchafu huu, ni kutokana na udhaifu wa katiba yetu unaompa rais mamlaka ya kuagiza taasisi zote za kimamlaka kufanya atakacho. Ukitazama wananchi waliopiga kura ni chini ya asilimia 35, na yote hayo ni sababu ya kupoteza imani na mchakato mzima wa uchaguzi, na yote haya ni kwasababu rais aliye madarakani ameweza kutumia madaraka yake kufanya kile kilicho ndani ya utashi wake.

Uchaguzi wa 2010 na 2015 respectively, tuliona uchaguzi wenye afadhali sio kwamba tume ilikuwa huru, bali wangalau ilijitahidi kuwa fair, Ila toka ameingia rais huyu hayo yamefutika. Na udhibitisho Ni kuwa wapiga kura walikuwa wanaongezeka, iweje sasa watu wakiwa na uelewa mkubwa, na idadi kubwa wapiga kura ndio wapungue ghafla? Ukitaka kujua kwa sasa kuna tatizo kubwa, angalia mitandao ya kijamii imefungwa hili Tanzania, vyombo vya habari vimedhibitiwa na ndio maana tunajadli kwenye jukwaa hili la jf Kenya na sio Tanzania.

Ndugu yangu. Acha kuhadaa watu
Waliojiandisha idadi -29million
Waliopiga kura- 15.5 million
Uncle Magu -13mill vote
Wabunge viti 264
Ccm - viti 262
Cuf -1
Chadema - 1
Madiwani -5200
Ccm -5200
Tatizo lenu ninyi wa chadema mnaongelea kwenye mitandao na wala hamuwafikii wananchi .
1;Mnakejeli barabara zilizojengwa ambazo mnatembeza magari yenu wakati wa kampeni.
2:Ndugu yenu zitto akakejeli kwa nini serikali inajenga hospital na kununua ndege haziwanufaishi wananchi. Matokeo yake alipopata ajali wakati wa kampeni akaenda kulazwa na kutibiwa katika hospital alizozikebehi,na ndio mteja mkubwa wa air tanzania kwenda kwao kigoma
3:Mkaja na hekaya za haki na uhuru wa kujieleza . Ndio slogan yenu. Tuliposikia hivyo tukajua tayari mnatumika,uhuru gani ambao mtanzania anauhitaji,uhuru tulipata 1961 toka kwa mabeberu.mtu anaamka vema,anaenda kwenye shughuli zake,hasumbuliwi sasa haki ya nini?
Hiyo ilikuwa ni tatizo lenu 2016 baada ya kupigwa marufuku mikutano ya siasa katika jimbo ambalo si lako mkaanza kulalamika haki.sasa wananchi hatutaki mikutano kwa hiyo slogan ya haki ilikuwa kwa ajili yenu na sio wananchi.
4:Hakuna mtanzania ambaye yupo tayari kuona kiongozi wake anakuwa controlled na mabeberu.Lisu katumwa na mabeberu .
5: Tanzania hatuungi mkono ndoa za jinsia moja, Tundu lisu alikuwa anaunga mkono ndoa za jinsia moja na pia mwanasheria wake ni shoga (gay). Robert amsterdam.(na point ya ushoga ndio iliyompotezea sifa)
6: hamjaibiwa kura ni watanzania wameamua kuwatandika viboko, mfano. Jimbo la kawe, askofu gwajima wa ccm kapata kura takribani 200,000 na halima mdee wa chadema kapata kura 30,000.
Pia mwenyekiti wenu mbowe katika jimbo la hai kapata kura 29000 na mshindi wa ccm kapata kura 99,000. Na huko ni vijijini na ni ngome ya upinzani.
7:katika kuwaonyesha kuwa magufuli anakubalika alikuwa akifanya kampeni siku 7, na baada ya hapo siku 7 anapumzika.so katika miezi miwili ya kampeni mwezi mmoja ameutumia kwa kupumzika.na pia hakuzunguka mikoa yote aliacha mikoa takribani 4 na ndio ambapo upinzani mkapata majimbo 2 ,kama angetia timu mngeondoka na 0.

8;na kwa kusema ukweli, uchaguzi ulikuwa huru,na wa amani.
9:tunamshukuru Mungu kwa kumaliza uchaguzi vema.

Sina chembe ya shaka ya nilichoongea. Halafu inaonekana unatumia nguvu huku ukijaribu kuweka data zisizo na usahihi.
[ol]
[li]Hakuna anayebeza barabara, usitake kuleta upotoshaji wa kijinga ili kubeba hoja zako za upotoshaji. Barabara zinajengwa kwa hela ya watanzania na wala sio hisani ya kiongozi yoyote, maana hata wakoloni walijenga barabara.[/li][li]Huu mchezo wa kuchanganya mambo ni ili kuficha ukweli wa hoja inayolalamikiwa, unachanganya ndege na hospitali ili kuficha malalamiko yalipo. Hakuna anayebeza hospitali, bali tuko wazi kabisa kuwa ndege sio kipaombele chetu, maana tuna mahitaji ya msingi kuliko ndege kwa sasa. Umeweka ndege na hospitali ili kuficha malalamiko yetu yalipo.[/li][li]Tulikuwa na uhuru wa kujieleza kuliko huu tulionao kabla ya awamu hii, je wakati huo tulikuwa tunatumika na nani? Sasa hivi tunajadili huku kwenye social media ya jirani zetu kisa huku kwetu social media zimezuiwa, mbona uchaguzi wa 2015 social media zilikuwa wazi, na bado hatukuridhika na matokeo, je ni shida gani ilitokea mpaka sasa social media zifungwe? Au uhuru wa kujieleza unaendana na utashi wa Magufuli?[/li][li]Hoja yako kwenye namba hii ni propaganda mfu. Ni kipi cha maana sana kipo Tanzania ambacho hao mabeberu wananikosa sehemu nyingine duniani, mpaka waone wamcontrol kiongozi wetu. Sio kila mtu ni muumini wa uzalendo wa mdomoni, sisi wengine ni waumini wa uzalendo wa moyoni, na sio wa kumsujudia kiongozi na mitazamo yake.[/li][li]Hoja yako namba tano ni utoto ule ule uliolishwa kisha unakuja mbele ya watu wenye akili zao na kuongea utoto uliolishwa. Misimamo ya Tundu Lisu iko wazi kuhusu jambo hilo, ila kwakuwa kuna kiwango fulani cha watu wenye uelewa duni, ndio maana mnatumia hiyo propaganda mfu kuwahadaa wananchi.[/li][li]Ukiwa hujui lolote na unaongozwa na ushibiki usio na tija unaweza kuamini matokeo hayo. Ila sisi tumeona kwa macho yetu nini kiliendelea. Kimsingi uchaguzi huu umetawaliwa na upikaji mkubwa wa matokeo, na matokeo yote kwa ujumla ni ya kushurutisha.[/li][li]Sijui hoja yako ni nini hapa, kwa maelezo haya inaonekana huna lolote ujualo zaidi ya kupiga propaganda mfu humu mitandaoni.[/li][li]Uchaguzi haukuwa huru bali wa vitisho na uoga. Na malalamiko ni uchaguzi kutokuwa wa haki.[/li][li]Kama uchaguzi umeisha vyema, ni kipi kinafanya social media zizuiwe mpaka sasa?[/li][/ol]
NB: Uandishi wako mbovu na figure zako za makosa, zinaonyesha uwezo wako duni wa ufahamu wa mambo.

Mtu yeyote mwenye akili timamu na mcha Mungu hawezi kuunga mkono mchakato mzima wa uchaguzi na matokeo hayo.

Wasimamizi wa vituo vya kupiga kura wanapojigeuza mamilioni ya wapiga kura lazima matokeo yawe kama haya tuliyoyashuhudia.Kura zilipigwa na wasimamizi maana turn up ya wapiga kura ilikuwa chini ya 30%,karibia kila kituo/jimbo ndipo hizo karatasi zilizobakia zikapigwa kwa wagombea wa CCM. Hesabu lazima ziharibike maana kwenye zile 30% wanagawana wote+70% ya kura Fake za CCM= ushindi wa aina hii tuliyoshuhudia.
Tulishuhudia ukiukwaji wa Haki za wapiga kura na kanuni/sheria za uchaguzi.Msituongopee kama ninyi mnaogopa ukweli,waacheni wengine wauseme.CCM mnashangilia matokeo ya uchaguzi Fake!

Unaambiwa kila kituo cha kupiga kura alipelekwa/walipelekwa watu maalum kufanikisha ushindi wa CCM.

Hata hivyo dalili zilishaonekana wazi tangu uchaguzi wa serikali za mitaa hadi uchaguzi huu kabla ya kura kupigwa wagombea wengi wa upinzani walienguliwa kwa makusudi kabisa. Can you imagine eti wagombea wote wa CCM hakuna hata mmoja aliekosea kujaza fomu ila upinzani tu ndio walionekana hawajui kujaza fomu.

Acha tuone wanachokwenda kufanya huko kutufikisha uchumi wa juu wakiwa peke yao maana upinzani kwao ndo kikwazo.

Nyinyi wenzenu wanakwenda kupiga kura nyinyi mnaelekezana kutumia VPN matokeo yanatoka mnajifanya hamyambui hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza shawishiwa na vibaraka vya mabeberu sasa JPM akishaapishwa tu hakuna siasa tunafanya kazi

Unaongea utoto gani boss, ukitumia VPN huwezi kupiga kura ama?

Ukweli ni kwamba nyinyi hamkupiga kura ila mlikimbilia mitandaoni mkidhani kule ndo kuna ushindi jambo ambalo si kweli tena ktk uchaguzi huu mmefanyiwa fair sana hamna wa kumlaimu zaidi ya nyinyi wenyewe

Hivi unadhani hatukuona kilichokuwa kinafanyika kwenye uchaguzi huu, ama unadhani tuko nje ya nchi. Kwa macho yangu nimeona mabox ya kura zilizopigwa na kuingizwa kituoni huku mawakala wa upinzani wakiwa hawapo. Watu wasiojua ukweli, au walioamua kuogopa kusema ukweli ndio wanaweza kuamini kuwa ccm imepata ushindi huu kihalali. Watu wengi wamepuuza huo uchaguzi ndio maana hawakujitokeza. Mengi ya matokeo yaliyokuwa yanatangazwa hayawiani na idadi ya wapiga kura waliojitokeza. 2/3 ya wapiga kura wamepuuza huo utoto uitwao uchaguzi.

Achana naye Shetani mkubwa huyo, watu tunastress wao wamefungia mitandao ya kijamii MUNGU awaangamize

Inasikitisha

Chama cha mapinduzi kimepata ushindi wa kishindo…