Tanzania na Burundi East Afrika tuna gundu gani?

[ATTACH=full]180461[/ATTACH]Kenya wanatengeneza magari,Uganda tena ya solar,sasa ni zamu ya Rwanda,kwanini sisi hatumo na tunapiga kelele kila siku nchi ya viwanda. Nchi inayovutia wawekezaji…kwanni hatupati mashavu kama haya?

Huwezi kuwa na taifa lenye ubunifu kama una kiongozi anayeamini katika mawazo tu ndio sahihi.

Zamani enzi za mwl. Tz iliwahi kuunda gari lake liitwalo Nyumbu kupitia JWTZ. Ubunifu ule ulifikia mwisho baada ya siasa kuwa sekta yenye mapato makubwa na njia ya shortcut kutoka kimaisha. Hakukuwa na haja ya ubunifu bali ujanja wa kuwa na receipt fake ili uibe hela ya umma.

Laiti kasi ile ya kuwapa wataalamu kipaombele ingeendelea leo hii tungekuwa na viwanda vyetu vingi vya magari. Lakini kipaombele kikapewa wanasiasa na leo hii kila mtu ni mwanasiasa kwani ndio shhughili inayolipa. Unashangaa mpaka mkuu wa nchi anahubiri yeye sio mwanasiasa lakini anapokelea wanasiasa wanaomuunga mkono kwenye hafla ya kijeshi!! Hao wanajeshi badala ya kujikita kwenye utaalamu kama wa kuunda magari wamegeuka vituko kila siku kuonyesha kuvunjiana matofali kifuani/kichwani kutishia wanaopinga watawala eti ndio ukakamavu.

Ni kweli sisi ni nchi ya vi-wonder

Sisi tupo kusifiana ujinga tu.

Miss bado haujafika

Namaanisha muda

Kiongozi wetu haaminiki hana msimamo wa a kueleweka…bora hata angekuwa anafuata sheria sasa maamuzi yanategea siku hiyo ameamkaje.

nlichogundua ni kwamba watz weng ni wanafiki, wakianza kutengeneza hapa tz tutasema hayo magar yanawasaidia nin wananchi wa kawaid ref sgr na ndege lkn yakitokea nchi za wenzetu tunasifia… tutanue akili kdgo.

sisi tunawasakama matajiri na wawekezaji kuwa ni wezi, tunataka wote tuwe masikini ili Dr magufuri awe na uwezo wa kutushawishi kwa kipande cha mkate tu. yule mzee ana mapepo sio bure

Taifa ambalo kila raisi ajaye anakuja na vimbaumbele vyake kamwe halitoendelea.

litaendelea kuwa hohehahe…

Mwinyi… Mzee wa Ruksa

Mkapa… Privatization

Jk… Sijui…

Ji×e… Sijui …bombrrdier.

…hovyohovyo tu.

Viwanda vyetu ni cherehani nne…

Cc: @Mahondaw

Ngojea tuwamalize wapinzani wakiisha tutaanza kujenga viwanda

:p:p:p

Viwonder Tanzania

Sisi tulitakiwa kuwa na kiwanda cha kubangua Korosho, kutengeneza pamba, kutengeneza majani ya chai, kutengeneza sigara na viwanda vya kusindika nyama na maziwa. Haya maswala ya kutengeneza Magari hayana tija

Wanaotakiwa kufanya kazi WaPo busy wanashabikia matusi ya Da’ mange na kutafuta haki ya kutukana mitandaoni

Ni swala la muda tu

Akili za upinzani wa kijinga ndo mawazo yao,akifanya kitu hata kma ni faida kwa wengi,utaona haina maana,akifanyiwa cha level yake ooh anabagua matajiri