Tanzania: DAR ES SALAAM PORT -Construction of terminals - Deepening and strengthening of Berths 1-7

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Ukandarasi ya kutoka nchini China inayofahamika kama China Harbour Engineering Company Limited (CHEC) kwa pamoja wamesaini mkataba wa kuanza rasmi kwa kazi ya maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (MB.) ameshuhudia tukio la uwekaji saini wa mkataba huku akisema kwamba ni historia kwa nchi yetu na kutoa wito kwa mkandarasi kuifanya kazi hiyo kwa weledi kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo na kamba Serikali haitavumilia ubabaishaji.
“Leo tunaanza kuandika upya historia ya Bandari ya Dar es Salaam ambapo tutashuhudia kazi hii ikianza na ujenzi wa gati la kuteremshia magari, kazi ya kuongeza nguvu na kuchimba kina cha maji katika gati namba 1 mpaka 7 pamoja na kuweka vifaa vya kisasa vya kupakia na kupakulia mizigo, pia tumemuomba mkandarasi apunguze muda wa ujenzi na kuteremsha bei na amekubali,” amesema Prof. Mbarawa.
Pamoja na hilo Waziri ameongeza kwa bandari kuwa na kina kirefu ni jambo moja na haitoshelezi ndio maana Serikali imeamua pia kujenga reli mpya ya kisasa ya SGR yenye uwezo wa kubeba mzigo mkubwa na kuwezesha treni kutembea kwa mwendo wa kasi zaidi wa kilomita 120 kwa saa.
“Kupitia reli hiyo mpya ya kisasa tunayoijenga (SGR), tunaamini tunaweza kushindana na bandari nyingine, nitoe mfano mdogo tu katika nchi jirani yenye bandari wao wamejenga SGR ambayo kusafirisha mzigo mpaka Kigali Rwanda (takribani kilomita 1,600) inawachukua saa 23 kufika Rwanda wakati kutoka bandari ya Tanzania mpaka Kigali (takribani kilomita 1,400) itatuchukua saa 13 pekee kufika Rwanda, jambo hili litawafanya Wafanyabiashara wengi kuitumia Bandari ya Dar es Salaam zaidi kutokana na kuwa na muda mfupi zaidi wa kusafirisha mizigo,” amefafanua Prof. Mbarawa.
Kwa upande mwingine Prof. Mbarawa amesema, “Nataka nitoe angalizo mapema kwa mkandarasi kwamba Serikali hii ipo makini (serious) na tunatarajia kazi hii itakamilika kwa kiwango na kwa mujibu wa makubaliano na hatutataka kuona viwango tulivyokubaliana havitekelezwi hatuvumilia jambo hilo hata kidogo,” amesisitiza Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko amesema, “Hadi kufikia mwaka 2025, TPA itaweza kuongeza mzigo kutoka tani za sasa milioni 14 kwenda mpaka tani milioni 28 mwaka 2022 na kama tusingejenga kwa mwaka huo wa 2022 tungeweza kuwa na tani milioni 20 kwa hiyo hii nguvu ambayo Serikali imeingiza itatuongezea ziada ya tani milioni 8,” amefafanua Eng. Kakoko.
Mradi huu umegawanyika sehemu mbili ambapo sehemu ya pili itahusisha kuchimba lango la kuingilia meli ili kupata mita 15. Sehemu ya kwanza inatarajiwa kuhusisha ujenzi wa gati jipya la kupakua mzigo wa magari (ro-ro), uimarishaji na uongezaji wa kina cha maji gati 1-7

[ATTACH=full]183354[/ATTACH]

[ATTACH=full]183355[/ATTACH]

[ATTACH=full]183356[/ATTACH]

[ATTACH=full]183357[/ATTACH]

[ATTACH=full]183358[/ATTACH]

[ATTACH=full]183359[/ATTACH]

vp ile ya bagamoyo washaanza ujenzi?

Nitaweka update hapa ili watu wajue soon.

Safi sana…

vizuri

Inapendeza sana…

Cc: @Mahondaw