Taarifa ya Uongozi wa JF umeleta tumaini jipya

Nimeiona taarifa ya Uongozi wa Jamji Forum ukisema kuwa watarudi hewani mapema kadri iwezekanavyo na imewashukuru wapenzi wa Jukwaa hilo maarufu la mtandao wa kijamii kwa kuwa wavumilivu

Nasi members wa JF tunawashukuru sana Uongozi wa JF kwa kuwa majasiri na kupambana na vitisho vyote vya utawala huu dhalimu usiotaka kukosolewa

Mungu ibariki Tanzania

ila tunaomba pia wabaki na huku kwani kuna usalama zaidi

Swala muhimu sana, Maana sasa ivi naona Jamii Forum aitakuwa Salama sijui Maxence Melo hataweza kuwaaminisha watu usalama wao au jukwaa LA siasa libaki uku. Kiusalama zaidi

Inavyoelekea hujapitia JF kitambo, hilo tangazo unalosema mbona ni la muda tu!, lina wiki sasa.

Sawa, inawezekana kwa upande wangu ndiyo nimeiona hiyo taarifa Jana tu…

tusubiri

Ndiyo hivyo mzee.
Tuachane na hayo, umesikia pia kuna forums kama JF imefunguliwa nchini Marekani?, inaitwa Bongo Forums, BF, wakuu kibao wameshajiunga.

Mm ntabaki hukuhuku

kajiungeni bongo forums… mambo yashakuwa magumu jf

Mie naogopa usalama wetu tu basi maana Mungu mtu wetu kadhamiria kweli

Ngoja niitafute.!

upepo unapita tuu

Basi wacha tuvumilie kwa kitambo

mkuu mbona sijaiona hiyo?ebu tupe nimecheck google mbn siioni?

Ila huku pia pametulia, japo naona kama wadau wengi kutoka JF bado hawajaja rasmi…shukrani kwa KT kutupa haki stahiki japo tuwakimbizi.

hii sawa kabisa yote ya yote nafikiri usalama utazingatiwa kwanza kwa sababu hata za kufunga zilikuwa ni hizo hizo usalama wa watumiaji kwanza mengine baadaye

Jamani naomba kujulishwa utofauti wa New villager. Villager na senior villager.

taarifa hiyo ni ya muda mrefu sana masharti anayopewa Mello ni magumu sana na yeye kagoma kutoa privacy za watu ni ngumu sana anasimamia anachokiamini

ni kama jf unavyoanza ,junior member ,senior member ,expert member wenzetu hapa wanatumia villager

mkuu ndio unanifungua macho wacha niitafute