Nimeisoma taarifa iliyotolewa kwa Umma na TCRA tarehe 16/6/2018 kwa kile ilichokiita upotoshwaji unaofanywa mitandaoni kuhusiana na kufungwa kwa mitandao ya kijamii na Blogs nchini Tanzania
Katika barua hiyo ambayo inakanusha kuwa mamlaka hiyo ya Mawasiliano hawana mpango wa kufuatilia wale wanaotumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram na tweeter
Barua ile ni ya upotoshaji mkubwa kwa kuwa tunajua kuwa watawala wa Tanzania wanafanya kila juhudi kuona kuwa hakuna mtanzaniia yeyote anayeweza kuikosoa serikali hiyo aidha ni kupitia kwenye vyombo vya TV na radio na Magazeti hapa nchini
Ni ukweli usiopingika kuwa hapa Tanzania vyombo vya habari vyote vya Umma na vya binafsi vimedhibitiwa vilivyo na mamlaka za utawala nchini Tanzania
Na vyombo vilivyothubutu kuikosoa serikali hii ya awamu ya 5 viliishia kupigwa faini au kufungiwa kabisa
Kwa hiyo watanzania kwa mamilioni wamekosoa mamlaka nchini ya kuingilia Uhuru wa TV na radio na magazeti ya Tanzania kutokana na vyombo hivyo kuwa na kazi moja tu ya kuusifu utawala wa Magufuli na serikali yake kuwa unatupeleka kwenye kula asali na maziwa!
Vile vyombo vilivyojaribu kuikosoa serikali hii ya awamu ya 5 walikiona cha moto!
Nitataja baadhi ya vyombo vya habari vilivyoonja joto ya jiwe, Mwanahalisi na Mawio ni mfano wa dhahiri ya namna serikali hii ya kidhalimu ilichowafanyia kwa kuwafungia maisha yasichapishe makala zake tena!
Kwa hiyo watanzania wakabaki na option moja pekee ya kupata habari zao “balanced stories” na si pengine Bali ni Jamii Forum, ambako nako makucha ya TCRA yamefika na kuwafungia, lengo ni kuwataka wamiliki wake wawajibike kwa mabandiko ya watumiaji wake!
Kwa hiyo hao TCRA wanafanya ghiliba kubwa chini ya utawala huu wa Magufuli wemye lengo la kuminya Uhuru wa vyombo vya habari ambao ni kinyume kabisa cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2005, ibara ya 18(1) inayotamka wazi kuwa " Kila raia wa Tanzania atakuwa huru kutoa mawazo yake kwenye chombo chochote na Uhuru huo haupaswi kuingiliwa na chombo chochote" mwisho wa kunukuu
Mungu ibariki Tanzania