SOMO: KUNA NJIA NYINGI ZA MAISHA! HUYU HAPA CRITIC WA DAZ NUNDAZ

Wanakijiji nawasalimu sana!

Anaandika SIMBA wa Morogoro, Afande SELLE!

@afandeseleking: Tukiwa hapa mjini Songea Mkoani Ruvuma, pamoja na kukamilisha majukumu yetu yote yaliyotuleta Ikn pia tukiwa pale ofisini kwa mkuu wa mkoa tukakutana na Ndg yetu wa kitambo Bwana Noel Kapinga au kwa jina la usanii tulikua tunamuita ‘Critic’.

Yeye ndio aliyekua muasisi na kiongozi wa kundi la muziki la Daz Nundaz na alishiriki kuchana ktk nyimbo zote kubwa za kundi lao kama ile Kamanda,Barua,Nipe tano nk…nk…

Sasa huyu mjamaa baada ya kipindi kile kuona kuwa mziki wa bongo figisu nyingi na haoni future hapo mbeleni akaamua kurudi darasani kupiga kitabu,alipomaliza akarudi kwao Songea ndipo akapata ajira kama afisa uvuvi hapa mkoani na ofisi yake jpo kwenye hili jengo la mkuu wa mkoa…

Na kupitia taaluma yake hiyo hajaishia kukaa ofisini tu bali akaenda shamba na kuanzisha mradi mkubwa wa serekali kuhusu ufugaji wa samaki wenye tija na kuwa kama ndio shamba darasa kwa
wamanchi wenye utayari wa kujifunza na hatimae kufaidika na fursa hii ya ufugaji wa samaki…

Basi kama wewe msomaji hujajifunza kitu chochote kupitia safari ya maisha ya critic, endelea kujiona shujaa, kwakua unakaa Dar na unajulikana kila Bar, ukifikiria fursa zitakufuata tu hata kama umekaa!

AFANDE SELLE & CRITIC
[ATTACH=full]182327[/ATTACH]

Hongera yake

Ni kweli anastahili Hongera

Wenzake kina Feruz na Daz wameishia kuwa mastaa wasio na kitu

hiyo ndo Akili ati sio unangangania kisicho riziki

Jamaa aliona mbali, ila sijui kama Afande Sele anachukua mkondo upi, au ataishia kusifia wenzake tu!..

Safi sana CRITIC.

Inapendeza…

Cc: @Mahondaw

Hongera Critic. Lakini uandishi wa Afande Sele unaonyesha jinsi gani alivyo na jealous na watu wanaofanya maisha yao Dar. Maisha ni kuchagua, kama yeye alivyochagua kuishi na kitambi. Sio lazima wote wakatafute maisha Impandelavua, kuna wengine wametoka huko kijijini wamekuja ku-win maisha Dar.