Nimemsikia Rais Magufuli akisema alipokuwa akitembelea ujenzi wa msikiti mkubwa wa BAKWATA hapo majuzi kuwa viongozi wa dini wasiruhusu wanasiasa kuwa ndiyo wasemaji wao
Naamini alilipiga hilo "dongo’ kuongelea ule waraka uliojipatia umaarufu mkubwa wa kanisa la KKKT uliotolewa wakati wa sikukuu ya Pasaka ya mwaka huu
Nimekuwa nikijiuliza hivi ule waraka ni kweli uliandaliwa na wanasiasa na baadaye ukasomwa na maaskofu??
Jibu nililolipata ni HAPANA kubwa sana kwa kuwa ninaamini kuwa waraka ule uliaandaliwa na maaskofu wa kanisa hilo kubwa hapa nchini la KKKT wakiongozwa na roho mtakatifu wa Mungu na waliweka na saini zao pale chini
Nimekuwa nikijiuliza je ni kitu gani kilichomfanya Rais ahusishe ule waraka na wanasiasa??
Jibu nililolipata ni kuwa Rais alipata kiwewe baada ya waraka ule kutoka, kwa kuwa yeye amezoea kusifiwa na kupambwa tu kuwa anawafanyia mema watanzania
Ule waraka ulikuja tofauti kwa kuwa ulielezea mapungufu mengi ya serikali ya awamu ya 5 ambayo serikali hii inapaswa iyafanyie kazi iwapo itataka nchi yetu iendelee kuwa na umoja wa kitaifa ambao tumeendelea kuwa nao tokea tupate Uhuru.
Umoja huo kwa Mara ya kwanza tumeanza kuona unatikiswa chini ya utawala huu wa Magufuli
Kwa hiyo kutokana na tamko lile la Rais ambslo naamini hakulitoa kwa Bahati mbaya ninadiriki kusema kuwa Rais amepotoka kwa kusema kuwa makanisa yana wasemaji wao ambao ni wanasiasa, ninachoamini Mimi ni kuwa makanisa yana wasemaji wake wenyewe ambao ni maaskofu wakiongozwa na roho mtakatifu wa Mungu na sivyo anavyotaka kutupotosha yeye Magufuli
Mimi mwenyewe nilishangaa sana,kwanini alitoa kauli ile…kwa kweli inabidi hawa viongozi wetu wakae chini waangalie ni wapi wamekosea…tunarudi nyuma sana kiuchumi,kidiplomasia,kimuunganiko kama taifa.
Yaani siku ile nilijua jamaa ni tatizo. Anaamini wanasiasa wana akili sana kuliko maaskofu kiasi kwamba maaskofu hawaoni tatizo lolote bali wanasubiri wanasiasa wawaelekeze cha kuongea! !
Kwenye sikukuu ya Iddi ndio nikaona mashehe Bakwata wakitema yale mashairi waliyomezeshwa na mkulu. Wao kazi yao ikawa kushambulia viongozi wa kikristo waliotoa nyaraka. Ni bahati taasisi ya kiisilamu ya kina shehe Ponda wametoa waraka stahiki kwa serekali hiyo jana.