Nianze bandiko langu kwa kunukuu Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, ya mwaka 1977, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2005, ibara ya 3 ambayo inasema hivi " Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania itakuwa ni nchi ya kidemokrasia, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu
Nimeanza bandiko langu kwa kunukuu kifungu hicho cha Katiba, ili tuone kwa vitendo na hulka yake huyu Rais Magufuli, kama kweli anafaa kuongoza nchi ya mfumo wa vyama vingi
Mara tu alipoingia madarakani, alionyesha dalili za kutotaka kukosolewa kwa kuondoa Bunge Live…
Akaja tena kupiga marufuku mikutano yote ya vyama vya upinzani hadi mwaka 2020…
Ndipo Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akatoa onyo mwaka Jana, kuwa huyu mtu akishamaliza kuumaliza upinzani atakuja kwenu CCM na kuhakikisha kuwa hakuna kauli yoyote ya kumpinga itakayotoka ndani ya CCM
Wakati ule alipoongea Tundu Lissu, wanaccm waliona kama ni “stories” tu za Tundu Lissu, lakini kutokana na kauli aliyoitoa Rais Magufuli kwenye kuapishwa kwa Waziri mpya wa mambo ya ndani, Kangi Lugola, ndipo alipothibitisha usemi wa Tundu Lissu!
Alinukuliwa akitoa onyo Kali sana kwa wabunge wa CCM wa mikoa ya Kusini, akina Hawa Ghasia na Nape Nnauye kuwa kama wabunge hao wangeendelea kuipinga serikali yake kupora pesa za wakulima wa korosho asilimia 65 za “export levy” angeanza kwanza kuwapiga shangazi zao hao wabunge wa CCM waliokuwa mstari wa mbele katika kuipinga hiyo Sera mpya ya CCM
Vile vile tumeshuhudia viongozi wakuu wa Chadema wakihangaishwa na kesi zisizokuwa na kichwa wala miguu, zenye Lengo la kutaka kuwafunga
Hivi hao viongozi wa Chadema wamefanya kosa gani iwapo nchi yetu ina mfumo wa vyama vingi na wajibu mkubwa wa viongozi wa upinzani ni kuikosoa serikali ili irudi kwenye mstari kwa manufaa ya nchi