Kwa wale tuliomsikiliza akilihutubia Taifa wakati wa kuapishwa kwa Waziri mpya wa mambo ya ndani, Kangi Lugola, aliyechukua nafasi ya mtangulizi wake, Mwigulu Nchemba, ambaye ametimuliwa uwaziri, atakubaliana nami kuwa, katika hotuba yake hiyo, Rais Magufuli amethibitisha kuwa Bunge siyo tena mhimili unaojitegemea, ambao wajibu wake mkubwa ni kuikosoa serikali kwa lengo la kutenda haki kwa wananchi wake, na badala yake amethibitisha kuwa Bunge hilo ameliweka mfukoni na analiagiza kutoka Ikulu kwa remote contro kwa yale anayotaka yeye yafanyike!
Siyo vyema kurejea kila kitu alichokisema, lakini nitanukuu baadhi ya mambo muhimu aliyoyaongea ambayo kwa kweli kwa maoni yangu hayapaswi kuongelewa na Mkuu wa nchi
Baadhi ya maneno aliyoyatamka ni kama yafuatayo:-
-
Nilisikia kwenye kikao kilichoisha cha Bunge baadhi ya wabunge wa CCM wakitishia kutoipigia kura ya Ndiyo bajeti hiyo, kwa kile walichokiita kuibiwa pesa za wakulima wao wa korosho na kutishia kuandamana iwapo pesa hizo hazitoridi. Waandamane tu na wakione cha moto na Mimi ningeanza kuwachapa shangazi zao ndiyo wajue kuwa Mimi siyo mtu wa mchezo mchezo!
-
Nilimuuliza Waziri Mkuu kuna wabunge wangapi wa CCM wa mikoa ya Kusini, akanijibu ni 17, nikamwambia Waziri Mkuu kuwa waache waondoke na watuachie CCM yetu na hatutayumba kwa kuwa bado koram ya kuongoza Taifa hili itakuwa upande wetu
-
Nilimwagiza Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru achukue mahudhurio (roll call) na nikaagiza kuwa wabunge wote wa CCM ambao hawatakuwepo wakati wa kuipitisha bajeti hiyo awalime barua za warning!
Nimekuwa nikijiuliza hivi hao wabunge wa CCM wa serikali ya awamu ya 5 hawana tena uwezo wa kuikosoa serikali yao, kwa mujibu wa Katiba ya nchi??
Kama wanao kwa kuwa wao ndiyo wawakilishi wa waliowachagua na wamewatuma wawasemee hayo waliyoyasema, nimekuwa nikijiuliza hivi kuna sababu zipi za msingi za kuwatisha wabunge hao/kiasi hicho??
Nimekuwa pia nikijiuliza, hivi akina Nape Nnauye na Hawa Ghasia ni wabunge wa kuchaguliwa na wananchi wa mikoa ya Kusini au ni wabunge wa kuteuliwa na Rais??
Ukipata majibu ya maswali hayo ndipo hapo utakapothibitisha kuwa Bunge limepokwa madaraka yake ya kuwa ni Mhimili unaojitegemea na hivi sasa umewekwa mfukoni mwa Jiwe na analicontrol kwa remote control akiwa pale Magogoni!
Ee Mwenyezi Mungu tufanyie wepesi wa kutuondolea huyu mtu ambaye hataki kabisa kabisa hata kule kupewa constructive criticism kwa lengo la kuijenga nchi yetu