Pizza

Jifunze kuandaa pizza nyumbani kwa recipe rahisi kabisa.

mahitaji

1.pizza dough (chapati)
Unga wa ngano
Chumvi
hamira

.weka unga katika chombo
.weka chumvi na hamira changanya
.weka maji kidogo kidogo huku ukichanganya unga, kanda unga ulainike kisha upake mafuta kwa juu ufunike uache uumuke.

2 pizza sauce
Mahitaji
Kitunguu saumu kiasi
Kitunguu maji 1
Nyanya 1
Carrot 1
Hoho 1
Mafuta

.weka sufuria jikoni
mafuta kiasi, katia kitunguu maji, carrots na hoho koroga.
weka kitunguu saum na nyanya pamoja na chumvi kidogo, ikiiva epua weka pembeni.

3 vitu vya kuweka juu ya pizza
Kitunguu maji
Carrots
Hoho cheese
Nyama ya kusaga ya ng’ombe , au kuku, au soseji au uyoga (kimoja utakachopenda)

Chukua tray ya kuokea ipake mafuta, weka unga uliokwisha umuka na uusambaze kwa mkono kutengeneza chapati (ukisukuma kwenye kibao haukubali ukiumuka unavutika kama bubblish hivo kuusambaza kwa mkono ni rahisi)
[ATTACH=full]179113[/ATTACH]

Choma /toboa na uma ili iive vizuri hadi ndani
[ATTACH=full]179114[/ATTACH]
Juu ya hiyo chapati pakaa sauce uliyoiandaa
[ATTACH=full]179116[/ATTACH]
Kwangua cheese juu yake, weka vipande vya kitunguu, carrot, hoho na nyama kisha cheese tena juu yake
[ATTACH=full]179118[/ATTACH][ATTACH=full]179119[/ATTACH]

Washa oven ipate moto kabisa
Kisha weka tray yako uoke pizza, 250 centigrade dakika 20 Pizza ipo tayari
[ATTACH=full]179121[/ATTACH]
Usipoelewa nakuja kukuandalia huko huko:p

Naomba offer kwa mujibu wa sentensi ya mwisho. Mimi huelewa zaidi practical

Offer imekubaliwa toa location

Ngoja nije pm. Ila inabidi iwe next weekend

Upo vizuri kama mentor

Na hyo margarine ya nn hapo pembeni?

Ya kupaka kwenye tray ya kuokea

OK got it…

iko vizuri