Ni nini hasa kimetokea kwenye sakata la Korosho?

Nasikia tu wananchi wameporwa 200bln na kupewa 10bln. Ni nini hasa kimetokea hadi imekuwa hivyo? ni pesa gani zimeporwa na kwaajili ya nini? zamani kwani ilikuwaje?. naomba kuelimishwa.

Anajua Nape Moses Nnauye na dada Hawa Ghasia

Siri kali huwa haipoli bali imechukua hela zake kwa manufaa ya umma; ni wakati muafaka wabunge wote wa kusini waombe msamaha kwa kuijaribu siri kali na kujaribu kukijeruhi chama kwani 2020 haipo mbali

Hii habari pia sijaifuatilia vizuri zaidi ya kusikia juu juu tuu, ngoja nifuatilie uzi huu hapa nijue yaliyojili huko kusini.

Kuna kitu kwangu hakijakaa sawa kwenye hili sakata la korosho. Nilitarajia ningepata tathmini ndogo ya maendeleo ya korosho toka huo mfuko umeanza. Ni kiasi gani kimewekezwa na tija ya kilichowekezwa. Hapo ningekuwa kwenye mazingira mazuri.

Kisheria 65% ya mauzo ya korosho ghafi nje ya nchi zinatakiwa zirudishwe kwa wakulima ili waweze kuendeshea Kilimo(Pembejeo, Semina na Saccos)

Hivyo majizi CCM yameamua kutozirudisha hizo zaidi ya Bil 200 na kufanyia mambo yao.

Ndicho kilichotokea mkuu.

Tukisema Jiwe na Maccm yake ni majizi watu wanatoka povu humu.

Miaka kadhaa nyuma baada ya kuona uzalishaji wa zao la Korosho unashuka mwaka hadi mwaka wadau wa korosho wakaitana ili kujadili kuliokoa zao hilo.

Kwa maana ya wakulima, bodi za korosho na makampuni ya ununuzi…katika kukutana kwao wakaafikiana kuwa katika kila mauzo ya korosho kuwe na ushuru wa kulilinda na kuliendeleza zao hilo.

Kwa maana hizo fedha zitatumika kwenye utafiti, uendeshaji, madawa na pembejeo zake kwa ustawi wa zao hilo.

Katika kujadili tatizo likaja nani wa kukusanya hiyo fedha?..ikabidi kupitia serikali waiombe TRA ndio awe mkusanyaji wao…TRA akawauliza mtanilipa nini kwa kazi hiyo… katika majadiliano wakakubaliana kuwa fedha itakayo kusanywa TRA atachukua asilimia 35 kama malipo yake na asilimia 65 itabaki kwenye mfuko wa uendelezaji wa zao la korosho…

Serikali ikatunga sheria ikapelekwa bungeni na kupitishwa.

Hali iliyopelekea uzalishaji wa zao la korosho kupanda kwa kiasi kikubwa kwa msimu wa mwaka jana.

Sasa awamu hii serikali ya Magufuli hata baada ya kuchukua asilimia zake 35, bado imeingia tamaa na kutaka kuchukua hata asilimia 65 ya wakulima ambazo ni sawa kisasa cha sh bilion 210…

Wanacholalamika wadau ni hizo fedha kutumika isivyo halali, kwa maana nyingine mwaka huu zao la korosho litakosa pembejeo muhimu kama misimu iloyopita…kifupi serikali imenyang’nya fedha za wakulima wa korosho…ambazo waliamua wenyewe kuzitoa baada ya kuona serikali imewatelekeza.

Hata baada ya serikali kukumbushwa na kamati ya fedha ya bunge kuwa hilo swala lipo kisheria…bado serikali imeenda kutunga sheria ya kujihalalishia hizo fedha… hata baada ya kushauriwa kuwa awamu hii iwalipe wakulima fedha na awamu ijayo ndio wafanye mabadiliko ya kujihalalishia fedha hizo bado serikali imeshupaa shingo.

.,…kwa jinsi nilivyo sikia na kusoma kwenye vyombo mbalimbali vya habari…kama nimekosea naweza kusahihishwa.

naona umeliweka vizuri km mh Zito alivyolieleza

Huu ulaji una wanene nyuma yake

Ilikuwa ni lazima kitokee kilichotokea, ni suala la muda tu…

Sakata la Korosho ni wizi wa mchana kweupe.

Hivi hii serikali kila kukicha ni kuja na sheria mpya tena sheria yenyewe ni ya kuwaumiza tu wananchi!!!

Dikteta ndivyo alivyo! Anataka akwapue pesa halali za wakulima wa korosho bilioni 130 ili azipeleke kwao Chato au aweke kwenye account yake binafsi.

Huu ndiyo upendeleo aliouahidi kwa mikoa ya kusini. Sijui hata kama anajua maana ya neno upendeleo maana hakuna upendeleo kwenye kuwapora wakulima wa korosho jasho lao la shilingi bilioni 130.

Dick - tetahaha magufool

Aliyepewa dhamana ya kukusanya ndiyo kazizuia zote…

Cc: @Mahondaw

siasa mchezo mchafu smart

Dah, kumbe hii ishu ni ya kionezi kiasi hiki? Kumbe anawapora pesa zao walizoamua kujiwekea kuendeleza zao lao???. Tanzania licha ya kuwa na ardhi nzuri kwaajili ya kilimo kamwe kilimo hakiwezi kuwa muajiri wa maana, kamwe hakiwezi kuendelea kwa huu wizi wa waziwazi kwa wakulima. Wenzetu Kenya nasikia waliogombania uhuru walikuwa ni wakulima wa cash crops. Walichofanya waliweka Tozo ndogo kwenye kilimo. Leo mkulima wa chai wa Kenya anapata hela karibu mara mbili kwa kilo ukilinganisha na waTz. Huko Rungwe watu wanang’oa chai wanapanda parachichi sababu ya hayo matozo na kuibia wakulima.

Huu wizi wa waziwazi kwa wakulima usiachwe upite.

Jamaa wangejua mapema wasingeipa TRA kuwakusanyia pesa. wangeipa hata benki binafsi.

Wenzao huwa wanawapa wakulima ruzuku yeye anawaibia mchana kweupe. Tatizo kubwa la kilimo cha Tanzania ni serikali kuwaibia wakulima kupitia Tozo. Zamani kulikuwa na ukabaila ambapo kabaila alimiliki ardhi kubwa na kukodisha wakulima wadogowadogo na kuchukua sehemu ya mazao yao. ulikuwa ni mfumo wa kinyonyaji. Leo serikali imekuwa kabaila. Haikodishii watu ardhi ila inachukua makodi makubwa yasiyoendana na uzalishaji.

Imagine jinsi hivyo 200bln zingekuza uchumi wa Lindi, mtwara na sehemu zingine?? Zingetengeneza ajira ngapi? wangapi wangehamasika kulima korosho. Waafrika hatujalaaniwa, ni ujinga na ulafi wa pesa tusizozitolea jasho ndiyo unaturudisha nyuma.

Criminal state! Sijui kama maamuzi kama haya huwa yanapata consencus ndani ya serikali.