Ni kwanini jezi za timu za taifa huandikwa namba nyuma na mbele na hazina matangazo ?

Kufuatia kombe la dunia linaloendelea na mashindano mbalimbali yanayohusu timu za taifa, tangu nimeanza kufuatilia soka, huwa naona jezi za timu za taifa zinaandikwa namba ya mchezaji kote mgongoni na mbele kifuani. Katika kufuatlilia kwangu nimepata maelezo tu kwamba mfumo wa kuwapa namba wachezaji ulianzishwa ili kurahisisha kuwatambua na kutofautisha kati ya mchezaji mmoja na mwingine katika matukio na masuala mbalimbali uwanjani na nje ya uwanja. Kwa ngazi ya vilabu tunaona namba zinaadikwa mgongoni pekee na lengo tajwa hapo juu linatimia. Je, ni kwanini katika timu za taifa namba huandikwa pande zote mbili ?

Na pia, ni kwanini katika timu za taifa jezi haziandikwi matangazo ya biashara vifuani kama tuonavyo kwenye vilabu ? Je, huku sio kupoteza mapato kwa kuiacha hiyo fursa ya kuwatangazia watu wenye biashara zao kupitia hizo jezi ?

FIFA wamemonopolize haki zote za matangazo!

Kwan timu za taifa wanalipwa mishahara???

Hivi ni sheria lazima iandikwe na mbele au ni maamuzi tu?

Ndicho ninachokiuliza hapa mkuu, kama ni hiyari je kwanini timu zote zinatumia jezi zenye namba mbele na nyuma, kwanini isijitokeze hata moja ambayo jezi zake zitaandikwa namba nyuma tu ?

Hawalipwi mishahara, lakini hiyo haitoshi ku"justfy" ni kwanini hawatangazi makampuni kupitia jezi. Licha ya kwamba hakuna gharama za mishahara, kumbuka kwamba kuna gharama za posho, gharama za kambi na maandalizi ya timu, vifaa, kuwalipa makocha na watumishi wengine wa timu na mengineyo yote hayo yanahitaji pesa. Bado swali langu linasimama palepale, karibu kwa ufumbuzi zaidi, lakini pia acha tuone wengine nao wana maoni gani juu ya hili

Kama ni hivyo, je kuna katazo lolote rasmi juu ya kutotangaza makampuni kupitia jezi za timu za taifa ? maana kama tatizo ni monopolization inayofanywa na FIFA kama ulivyoongea, je inakuaje kwenye mashindano ambayo wao FIFA wanakua hawayaratibu moja kwa moja mfano CECAFA challenge cup, na mengineyo… ?

Ninatambua kwamba FIFA ndio wenye mpira wao, lakini je hilo ni katazo rasmi ? Nina uhakika hata leo hii Taifa stars wakicheza mechi ya kurafiki na Harambee stars (mechi ya kuuenzi urafiki wa Mwl Nyerere na Mzee J. Kenyatta let say) bado kwenye mashati yao hakutakua na matangazo ya biashara… Karibu

Hakuna mechi yeyote ya kirafiki ambay haina wadhamini,iwe inatambuliwa na FIFA ama la

Zile zinazotambuliwa na FIFA wadhamini huwa chini ya uongozi wa FIFA ikiwa na maana mpunga unawekwa huko kisha kila timu huwa na gawio na kitu pekee kitakachotambulosha udhamini ni mipira inayotumika au matangazo pembeni ya uwanja lakini pia suala la biashara kupitia mpira wa nchi na nchi sio lengo kuu la kuanzisha mashindano ya kimataifa ndio maana hata wachezji hawalipwi yani ni kama kudumisha mahusiano tu ya walimwengu na watu kujiona wapo sawa uwe mzungu au mwafrika…

Asante kwa majibu yako mazuri, lakini ninadhani pengine haujanielewa nataka kujua nini, sijazungumzia wadhamini wa jumla wa mashindano au kwenye mabango ya uwanjani. Mimi nauliza kuhusu ni kwanini matangazo ya makampuni hayawekwi kwenye jezi, au ukipenda ziite fulana, au T shirt au ukipenda yaite MASHATI. Labda nitoe maji na mifano kidogo, kwenye “SHATI” (jezi) ya Simba/Yanga/Singida Utd kuna SPORT PESA wanajitangaza kupitia hapo, Man Utd wanawatangaza CHEVROLET, Chelsea wanawatangaza YOKOHAMA, Arsenal, Real Madrid, PSG wana FLY EMIRATES n.k

Swali langu ni je, kwanini kwenye MASHATI ya timu za taifa mfano Taifa stars (Tz), harambee stars(Kenya), super eagles(Nigeria), three lions (England), Seleçao (Brazil), Azzuri (Italy) na zingine zote hapatumiki kwa ajili ya matangazo hayo ?

NB; Nazungumzia jezi rasmi za mechi sio kwenye mazoezi.

NBB; Usinambie kuhusu mabango tafadhali maana hata Old Trafford pana mabango kibao lakini hayazuii CHEVROLET kuuza sura kwenye matumbo ya akina POGBA na wenzake … Karibu.

Nadhani na wewe hujanielewa

Kwa uelwa wangu mdogo ni kuwa nchi ni mhimili wa kiungozi na popote uionapo timu ya taifa inamaana inawakalisha taifa husika na serikali yake hivyo hakuna nchi yenye sponsor

Namaanisha huwezi kuchukua jezi ya Tanzania ukapachika VISiT RWANdA au UGANDA ukapachika FLYemirates hiyo itafanya kuonekana serikali yako iko chini ya kampuni flani

Kumbuka serikali ya nchi husika ndio humiliki timu ya taifa dats why kila iendapo inakuwa na Bendera ya Taifa la nchi husika kama mwakilishi…

Kama hujaelewa basi Aisee

NBB; Usinambie kuhusu mabango tafadhali maana hata Old Trafford pana mabango kibao lakini hayazuii CHEVROLET kuuza sura kwenye matumbo ya akina POGBA na wenzake … Karibu.
[/QUOTE]

Unapokuwa unauliza kitu jaribu kutokumpangia mtu cha kukujibu hata kama anachokujibu unakielewa vumilia na msikilize waeza ambulia kitu katika majibu yake

Wakijibu watu majibu tofauti hapo ndipo unapata nyongeza ya jibu kamili la swali lako

Acha tu nikuelewe kwamba timu hazifanyi matangazo kwenye jezi kwa sababu timu za taifa ni mali za serikali. Lakini nakuacha na take home note kwamba kama suala ni “kuwa mali ya serikali” kuna hizi klabu ni mali za serikali na zinatangaza biashara za watu kupitia jezi kama kawaida. URA na KCC za Uganda, Mbeya city fc, Tanzania Prisons, JKT ruvu na nyinginezo kibao. Sijui inawezekanaje wadhamini wao wakawa juu ya mamlaka za serikali zinazomiliki timu hizo. Asante kwa mchango wako mkuu

Unapokuwa unauliza kitu jaribu kutokumpangia mtu cha kukujibu hata kama anachokujibu unakielewa vumilia na msikilize waeza ambulia kitu katika majibu yake

Wakijibu watu majibu tofauti hapo ndipo unapata nyongeza ya jibu kamili la swali lako
[/QUOTE]

Lengo langu halikuwa kukufundisha namna ya kujibu, hapo nimejaribu tu kueleza ni kwa namna gani nina maono na maoni tofauti juu mchango wako hasa kwenye kipengele hicho mahususi kilichonukuliwa. Katika mjadala wowote ule ni kawaida kabisa watu kutofautiana kimawazo na kimtazamo. Sitokuwa sawa kama nitakubaliana na kila kitu bila kuhoji ukweli wake eti tu kwa sababu mwenye mamlaka ya kujibu ni wewe. Sina ubaya wala ugomvi na wewe kabisa, lakini ninaweza kuwa na ugomvi au hata vita na hoja na majibu yako kama naona kuna kitu pengine hakiko sawa. Asante

Ulishawahi kusikia hisa za timu ya taifa ya Tanzania zinauzwa kwa mtu au kikundi cha watu?!

Uliwahi kusikia timu ya taifa ya Tanzania inasajili wachezaji kutoka Rwanda au Burundi?!

Fuatilia timu za ligi kuu uingereza baadhi hazitoki uingereza ni pembeni huko…

Chief jibu hoja ambayo umechanganua vyema
Kifupi Simba anaweza kuomba kushiriki ligi kuu Kenya ila Tanzania haiwezi kuwakilishwa na Kenya

Unaweza kuanzisha klabu yako ya mpira hata kesho ila unalipa mapato ndani ya serikali na timu yako haiwezi kuwa ya serikali

Hizo ulizozitaja zilianzishwa na Taasisi za serikali miaka hiyo ya nyuma watu hawajui soka na ilikuwa ni kama kuporomoti tu lakini pia michezo mingi ilikuwa chini ya serikali hadi mabondia lakini sasa mambo hayo hamna zote hizo saiz zina wanahisa maana si mali tena ya serikali na serikali inatimu moja tu Ya Taifa

Fikiria upya ili mjadala uishe

SAWA

Ni rahisi kwa mtangazaji wa mpira kwenye TV kuwatambua wachezaji

Vipi kwenye vilabu ambako hakuna namba upande wa mbele, watangazaji wanapata ugumu wa kuwatambua wachezaji? Kumbuka kwamba namba ya kwenye bukta inaonekana vizuri tu upande wa mbele kurahisisha utambuzi huo.

hizo timu zipo chini ya taasisi za kiserikali lakini inajiendesha kibiashara timu ya taifa haijiendeshi kibiasharaa