Jamani naskia raha nasia amani hakika nafurahi kuingia tena humu ambapo sisi kama wana Jamii wa hii Forum tulijiunga miaka hiyoo na hakika kadiri nyakati zilivyo pita tumeendelea kuona Jamii Forum ikikua na kuboreshwa kila inayoitwa leo,kwakweli baada yakupata fununu kwamba Jamii Forum inapatikana Kenya Talk nilifurahi na fasta nikaigoogle hatimae nimefika ingawa nilipata changamoto kidogo kwenye kuwa registration neno REcupture…lilinitoa jasho,Mungu ni mwema nikajiunga kupitia Facebook na hatimae nimefanikiwa.
Hongera Max Hongera sana.
Hongera na hongereni nyote pamoja na timu yako ya ufundi na hata Wanasheria wa Jukwaa hili…niseme tu hakika MUNGU SI MWANADAMU HATA ASEME UONGO,Ni kweli sauti ya wengi ni sauti ya MUNGU.
NASKIA RAHA SANA NDUGU ZANGU,yani nipo Tanzania lakini Nafsi na Mwili wangu naouna kabisa unakata mitaa flan flan hivi ya Nairobi…
Nawashkuru mno Wakenya Hasa KENYA TALK kwa kukupa (CHUMBA CHA UANI:):)) walau tumejihifadhi kwa muda kutokana na maafriko yaliyo tokea huku shambani kwa bibi linalomilikiwa na CHama cha mapinduzi yaani ccm ambapo Mwenyekiti wake ni stone,yani Jiwe ambalo lililokataliwa likawa Chuma chakavu…yani kila kikitaka kujinyoosha kinakaza…kikijitahidi waapi kinajikaza mwisho Watanzania tumekuwa kama WABABELI,hakuna lugha ya kimaendeleo tuiongeayo ikafanikiwa…Vurugu tu kila kukicha,Mauaji,Utekaji,Wizi wa Fedha Zetu 1.5,unyongaji wa habari,Bunge wamejimilikisha,Bombasweet:p:pnk…kwakweli yani ni Kero kero kuu kwenye hii Nchi.
Hakuna lisilo na mwisho na mwisho wake ni Mbaya zaidi ajuavyo yeye…hakika Mwisho wake ni mbaya mno…ni sawa tu yeye aendelee kujihesabia haki akidhani Watanzania wote hatuna AKILI,
Sikutarajia hakia
MAGUFULI LEO HII AMETUFANYA TUMEKUWA WAKIMBIZI WA NAFSI…YAANI KIMWILI TUPO TANZANIA LKN KIROHO TAYARI TUPO KENYA…TAYARI NI WAKIMBIZI…BADO TU SEHEMU YA MWILI AMBAPO(ROHO NDIO ITIAYO UZIMA ,MWILI HAUFAI KITU)
Mungu awabariki WanaJf wote,
salaam zenu watoto wa mama mdogo wote mliomo huku kwa hila(LUMUMBA FC)