Nani kaelewa agizo hili la waziri mkuu Kassim Majaliwa?

[ATTACH=full]180801[/ATTACH]

Hujaelewa nini, si mmeambiwa watumishi marufuku kulala na magari ya serikali nyumbani kwenu…

Nini maana ya Magari yote ya serikali? Tena anasisitiza yoote.

Mkuu inaonekana umemwelewa zaidi unaweza kutufafanulia…

Alisema magari yote Serikali yalazwe kwenye yard ya Afisa Usafirishaji.

Gari zote za halmashauri muda wa kazi ukiisha yapakiwe kwenye Yard ya Serikali na sio sijui mtu anaenda kulala nalo nyumbani kwake au guest.

Kwahyo sasa hivi weekend hatutaziona katika parking za bar

kwahiyo unataka kusema mfano mkoa wa mara ikifika jioni gari ya mkuu wa wilaya ya serengeti imepelekwe kulazwa kwenye yadi ya afisa usafirishaji mjini Musoma, au kwa mkoa wa Simiyu gari ya mkuu wa wilaya ya Busege jioni ipelekwe bariadi

Pikipiki je???ngoja nikatambe na pikipiki ya serekeli weekend hii kabla hawajabana

serikali matamko ni ngumu sana kuwaelewa

Mkuu Idawa1 kama ww ni mzoefu hii amri si mara ya kwanza ndani ya nchi hii na mara zote imekuwa ikigonga mwamba. Ni kwanini hii amri itakufa kifo cha mende? viongozi wanaopaswa kusimamia hii sheria ndio vinara wa kuivunja.

Hao walioshangilia mi ndo nawashangaa… Wameshangilia nini labda!?

Mkuu, unamaanisha kuwa ofisi ya mkuu wa wilaya ya tarime haina afisa usafirisha?

Hapo kwenye Yoote kuna ukakasi, namaanisha haiwezekani magari yote ya serikali yasifanye kazi usiku! Yaani haiwezekani hata siku moja.

Nani kaongelea mambo ya tarime? au wewe ni mmoja wa waliokoswakoswa na pyu pyu ya zakaria

Nilimaanisha serengeti mkuu!

Yale mambo ya zakaria sio mchezo

Waziri Mkuu anajidhalilisha bure, amri yake haitekelezeki!

hiyo ndiyo Micromanagement. Huyu alitakiwa awe anafanya mambo ya maana kwa nchi. Hizi ishu ndogondogo awaachie wakuu wa wilaya.

Hii ngumu kutekelezeka kwa baadhi ya watumishi

Hata kama kuna hiyo karakana, tuseme mtu yuko seronera ambayo ni km 90 toka makao makuu ya wilaya kwenye hiyo karakana na jioni imefika ina maana aendeshe km 90 akapaki gari halafu kesho yake aanze safari tena kwenda kuendelea na alichokuwa anafanya km 90

Hayo matangazo ni miaka mingi sana yanatolewa hata jiwe mwenyewe aliyatoa sana akiwa waziri lakini wapi!!na hilo suala eti watumshi wote waishi katika vituo vyao vya kazi huu ni mwaka wa pili namsikia kila mala ila mbona bado halijaisha!!kuna vitu vingine utekelezaji wake wanajua ni mgumu ila ni kusema tu