Mwas na bahati mbaya

Kuna hawa wasee huanga na bahati mbaya. Ni wasee wenye shida na bahati mbaya huwafuata tu kila mahali. Kuna morio wangu huitwa Mwas huyo msee na bahati mbaya ni kitu moja.

Kuna day tukiwa tao huko OTC tukitembea kuenda bus station, Mwas alishikwa tu na karau random manze akapigwa mabare ka zote. Nikaskia akishow karau “Pole sana afande”. Karau akamchorea kumuuliza rada ni gani mbona anapigwa mabare msee ananishow hata hajui ngori ni gani.

Day ingine tulikuwa tu baze tumetulia tukichoma weed. Tulikuwa mtu tatu; mimi, mwas na msee mwingine anaitwa ndoch. Tulichoma blunt ya kwanza tukamaliza, tukachoma ya pili ikaisha. Tukiwa ya tatu nikaskia kunyora nikaenda kumwagika hapo nyuma ya hiyo baze. Ndoch alikuwa ameenda shop kushika tools za kuchana jaba. Nikiwa namwagika naskia, “Kijana wewe ndo unavuta bangi hapa”, kuchungulia kwa shimo ya mabati nacheki mwas amedandiwa na makarau wawili watiaji mbaya, mmoja anaitwa onyi na mwingine anaitwa kasee. Walikuwa na plain hungewanotice. Ilibaki nimechill hapo nyuma ndo nisidandiwe pia. Ndoch pia kuona ivo akaenda baze ya pool ndo ngori iishe. Ilibaki tumechangia Mwas 10k ndo aachiliwe na makarau.

Kuna day ingine tukiwa kwa stage tukichill tu, Mwas alichokozana na ma ngororia (wasee wa kuchota mchanga). Ilikuwa ngori manze juu huyo ngororia alichokozwa na mwas alichapa Mwas spade ya shingo Mwas akaanza kubleed ile noma. Tulimkimbiza hosi bana ndo atibiwe asidedi.

Kuna day ingine tena pale stage Mwas akiwa anajaza gari ya kuenda tao alidandiwa na karau juu ya touting. Huyo karau alijifanya ati ye ni customer Mwas before amjibu pap akapigwa pingu next alipelekwa industrial area akakaa wiki mbekse. Ilibaki amechangiwa 20k ndo aachiliwe.

Kuna day ingine pia Mwas alipewa mat aamke nayo ngware before donda main aamke. Huskii hakufika tao. Alidandiwa pale stadi juu hakuwa na badge. Ilibidi tumchangie 3k aachiliwe manze.

Alafu kuna day flani apo, kuna msee anaitwa maich alikuwa amechunana tenje. Sijui alichunana wapi. Huyo maich anakuanga dingo ile mbaya. Huyo akikuitisha kitu usimpee. Kuna day aliitishanga tenje ya ndoch ati anadai kuvutia mathake ivo ndo alipotea nayo manze. Jamaa kumbe iyo siku alisonga nayo alafu akaiskuma very fast. Saa hiyo day maich alikuwa amekam na ki samsung kimeweza bana. Iyo idhaa mwas hakuwa na tenje. Akaitisha maich hiyo samsung aeke sim card avutie mokoro wa kwake. Huskii alieka sim card tu ivi alafu akadandiwa na makarau walikuwa na plain clothes. Kumbe tenje ilikuwa inatrackiwa bana. Mwas hapo alishindwa kujitetea manze. Utajitetea aje na umepatikana na tenje ya udingo kwanza ikiwa na sim card yako ndani. Mwas alikuwa anadai kuekelea maich lakini kuna venye maich aliruka hiyo story bana akadai hata atambui Mwas. Ilibaki Mwas amedoze stenje mwezi moja ndo huyo dem aliibiwa tenje akadrop charges msee akaachiliwa.

Juzi juzi tu last month, tulipata mwas na bandage kwa kichwa. Kumuuliza rada ni gani akatushow ati jana yake magizani akienda mtaani zake zikiwa zimeshika kuna majamaa walikuwa wanapita na senke alafu mmoja wa hao wasee alimwekelea rungu ya kichwa jamaa akachanganyikiwa hadi zikashuka. Msee alitushow alibleed kama si ndoch kumpata kwa roadi na kumpeleka clinic, msee angesonga very fast.

Mwas na bahati mbaya ni kitu moja.

Transleshen please :D:D

U is a very good story teller

Copyright this shot, nigga

Good story

Reminds me of African short stories. Crazy book

Class two children in China are making robots and then you have these… Mwas bonobo ndoch smoking weed and stealing meat

and what have your children invented so far?

Nyinyi ndo mko na bahati mbaya kuwa na beste Ka mwas…
Unadhani yeye huskia poa aje kujua ako na maboyz anaweza tegemea ata kuende aje, mtamtoa Kwa ngori…

Senke ni nini?

Hiyo pia tu ndio sijashikanisha

nduthi

Hapa imebidi nicheke :smiley:

Bana. Kupata mabeshte kama hao si rahisi.
He’s one lucky mofo.

Mwas must bearing the countenance of a criminal (protruding eyes, sumken cheeks, cracked lips, dry skin and shaggy hair) being a smoker and a frequent user of intoxicating products.

He is thus easily profiled as a suspect for possession.

:D:D:D:D tuhekaya tusafi mkuu.

safsana

Hii hekaya… Mwas aokoke tu

:D:D:D

One mungu anapenda huyu morio wenu vibaya sana.hadi kifo inaogopa bahati mbaya.

Huyu Mwas ako na swara joh, inakaa alizaliwa siku mbaya.