Muuaji wa Lissu lazima ajulikane

ANAANDIKA TUNDU LISSU…

Akida Deo Siwalile watahojiwa lini??

Nimemsikia Mwita Mwikabe Waitara na alichokisema juu ya jaribio la mauaji dhidi yangu la September 7 mwaka jana.

Sijashangazwa hata kidogo na maneno yake. Amerudi kwenye madhehebu yake ya zamani, lazima ajionyeshe ana msimamo mkali wa kiimani kuliko wale aliowakimbia mwanzoni na ambao sasa amewarudia.

Nilishambuliwa nikiwa na dereva wangu. Niliwaona walionishambulia kwa macho yangu mwenyewe.

Niliona alichofanya dereva wangu kuanzia risasi zinarushwa mpaka aliporuka nje ya gari na kujificha.

Niliona jinsi yeye na mfanyakazi wangu wa nyumbani wakisaidiana na mfanyakazi wa Naibu Spika Tulia walivyonitoa kwenye gari yangu na kunikimbiza hospitalini kwenye gari ya mfanyakazi wa Naibu Spika Tulia.

Mimi ndiye niliyemwagiza ampigie simu Mwenyekiti Mbowe na wabunge wengine wa CHADEMA wakati wananikimbiza hospitali. Nilikuwa na fahamu na nilikuwa nazungumza mpaka nilipoingizwa theatre Dodoma General Hospital.

Nimekaa na dereva wangu miezi minne Nairobi Hospital. Polisi walileta ujumbe kwamba wanataka kuja kunihoji mimi na dereva wangu.

Tuliwaambia waje. Hawakuonekana mpaka tumeondoka Kenya na kuja Ubelgiji. Leo hii ni miezi saba tangu tuje Ubelgiji. Hawajaonekana.

Tuna uhusiano wa kibalozi na Ubelgiji wa miaka mingi. Wana Ubalozi kwetu na tuna Ubalozi hapa kwao. Serikali ya Magufuli haijaomba msaada wa Serikali ya Ubelgiji ili utaratibu wa kumhoji huyu dereva au mimi mwenyewe ufanyike.

Tuna sheria iliyotungwa na Bunge letu inayoitwa Mutual Assistance in Criminal Matters Act, ambayo imeweka utaratibu wa nini kifanyike mtuhumiwa wa jinai au shahidi anapokuwa kwenye nchi nyingine. Hakuna mwenye habari nayo.

Jeshi la Polisi la Tanzania ni mwanachama wa Interpol (International Police Organization) ambayo inaweza kusaidia upelelezi wa jambo hili. Interpol nayo imesahaulika.

Dereva wangu amesafiri mchana kweupe kutoka Dodoma hadi Nairobi. Ametumia hati ya muda ya kusafiria iliyotolewa na watumishi wa Idara ya Uhamiaji ya Tanzania mpakani Namanga.

Amekuja Ubelgiji kwa hati ya muda ya kusafiria iliyotolewa na Ubalozi wa Ubelgiji Nairobi kwa sababu hati ya muda ya Tanzania ilikwisha muda wake.

Anaishi Ubelgiji mchana kweupe. Niko naye muda mwingi. Aliyekuwa Balozi wetu hapa na maafisa Ubalozi wa kwetu wamenikuta naye hospitali. Nimemtambulisha kwao.

IGP Sirro alishasema hadharani kwamba Jeshi la Polisi limefunga faili la upelelezi juu ya kushambuliwa kwangu. Polisi wanajua kilichofanyika, ndio maana hawajawahi kuhangaika na taratibu hizi za kufahamu ukweli.

CHADEMA na familia yangu tulidai uchunguzi huru wa shambulio dhidi yangu. Tulisema Serikali ya Magufuli na watu wake wanahusika na jaribio la mauaji dhidi yangu. Hawawezi na hawataweza kujichunguza.

‘Watu wasiojulikana’ walitumwa na Magufuli na watu wake kuja kuniua. Ndio maana ulinzi wote Area D ninapokaa uliondolewa siku hiyo.

Ndio maana CCTV ya kwa Waziri wa Nishati Medard Kalemani iliondolewa baada ya tukio.

Ndio maana Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ilizuiliwa kuwasilisha taarifa yake bungeni.

Ndio maana Magufuli aliwakataza Wabunge wa CCM na viongozi wa serikali kuja kuniona hospitalini Nairobi.

Ndio maana amekataza Bunge la Spika Ndugai kunitibu kama inavyotakiwa na Sheria ya Uendeshaji wa Bunge.

Ndio maana sasa tunasikia kwamba mara baada ya kushambuliwa, Magufuli aliwaelekeza Mawaziri Mwigulu Nchemba na Augustine Mahiga kukanusha hadharani kwamba Serikali yake haikuhusika na jaribio hilo la mauaji.

Ndio maana tunasikia Magufuli alitoa maagizo, mara baada ya kushambuliwa kwangu, kwamba nikifariki dunia mwili wangu ukimbizwe haraka kwetu Ikungi, Singida, kwa maziko; kusiwe na shughuli yoyote rasmi bungeni Dodoma, na kwa vyovyote vile nisipelekwe Dar yaliko makazi yangu.

Ndio maana mpaka sasa Magufuli, huyu anayependa kuonekana mcha Mungu na mwenye huruma, hajawahi kuonekana akisema chochote juu ya shambulio hilo.

Anawajua fika aliowatuma kuja kuniua. Jeshi la Polisi linawajua. Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi inawajua. Wanawaita ‘watu wasiojulikana’ lakini wanawajua fika.

Haya ya akina Waitara ni majaribio tu ya kupotezea kuhusika kwa Magufuli na Serikali yake. Lakini kama nilivyosema majuzi, sooner or later, ukweli utajulikana tu.

Habari zaidi, soma => DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Hili jambo si dogo, IPO Siku Watanzania tutakuwa pamoja na kudai haki na wadhalimu watawajibika.Sio mbali kwa kazi ya polepole na boss wake kuhalalisha biashara haramu.

Kumbe Yohana alikuwa na funera arrangements lakini hakuwa na plan B just incase

Unategemea awe na plan B wakati hana plan b ya ugonjwa wake

Mmh

Kule JF comments zinafutwa JF is no longer where we dare to talk

Mimi nilidhani peke yangu ndio nimeligundua hilo. JF sio kabisaa. Full upuuzi.

Kule TZ ni mavi tupu. Siwapendi katu. Wanajifanya wanatetea uhuru wa habari kumbe hamna lolote. Sasa hivi wamekuwa hovyo mwanzo mwisho! Ukiangalia mwonekano wa JF TZ ni sawa na hapa wamekopi toka huku

Daaah
Muda utasema tuu!!

Aisee! Nyerere aliposema mtu yeyote mwadilifu (mchamungu) hawezi kupakimbilia ikulu alimaanisha haya, maana yeye mwenyewe alikaa hapo ikulu miaka 23, anajua aliyoyafanya kabla hajatubu hadharani… Lakini huyu mwingine kila siku anaomba tumuombee utadhani kalazimishwa kuendelea kukaa hapo ikulu!.. :oops::oops::oops:

Ni kweli dada

Hiyo title mbona kama inamchulia jamaa yenu??

Msalimie Jiwe.

Mwambie Mungu hazihakiwi

muuaji anafahamika labda mfyatua risasi

Jiwe ndiye muuaji , mfyatua risasi ni Bashite &Co. Ltd including Jerry Muro

Hakuna cha kumchulia, muuaji ni jiwe, anafahamika.

Time will tell…

Cc: @Mahondaw