Msaada, Jinsi ya Ku - "Rotate" Saved Video

Wakuu kwema?

Kuna Video nilimuomba mtu akanirejodie kwenye tukio moja hivi, but aliweka simu Upande. So hata Nilivyozihamishia kwa Laptop zimetokea zikiwa zimelalia upande mmoja. Now nataka nizi-rotate ili zikae wima, hapa nafanyaje wakuu??

Ingekua ni Picha za Mnato najua ni rahisi tu, just right click then rotate, but hapa ni Video hizi.

Mimi ninachojua ni mpaka niiweke kwenye timeline ya program ya editing (final cut, Adobe Premier au Adobe Aftereffect ndiyo niirotate…

hapo hata uki rotate aspect ratio itaharibika. mfano kama alirekodi kwa wima uki rotate ikae mlalo watu watakuwa vibonge. kama alirekodi mlalo uka rotate wima basi watakua wembambaaa.

kama alivyosema mdau video editor nyingi zinaweza kurotate ungetaja kifaa unachotumia na possible os yake ungesaidiwa software.

Nilitumia simu ya kawaida tu ya Android, sasa nataka ikae kwenye Laptop syystem ya Window

software rahisi ni windows movie maker, hii inakuja na laptop, click start kwenye laptop yako kisha jaribu kui search ipo?

Kwangu haipo hiyo Mkuu, labda nii download

ni windows ngapi unatumia?

test hii
https://filehippo.com/download_windows_live_movie_maker

utaenda tu edit kisha rotate.