mobile network companies in tanzania should pull up their socks, bakhresa is coming to invest in same sector.

sote tunajua kilichoipata dstv baada ya bakhresa kuazisha azam tv(azam pay tv).

hakuna ubishi kwamba azamtv ni moja kati ya kampuni za paytv inayotoa huduma zake kwa bei nafuu na kwa ubora mkubwa nchini tanzania kiasi cha kuwa na wateja wengi katika kila mkoa.

sasa ni rasmi, bakhresa yupo katika maandalizi na hatua za mwisho za kuanzisha kampuni itakayotoa huduma za simu za kiganjani.

huduma zake hazitokuwa tofauti na vodacom,tigo, zantel au safaricom ya kenya.
hivyo basi, makampuni hayo yajiande kisaikolojia kabla ya kukumbana na mvumo wa radi uliotokea kwa kampuni ya dstv.

kwa mujibu wa msemaji wa makampuni ya bakhresa, kampuni hiyo itafahamika kama
azam telecommunication tanzania limited.

https://www.youtube.com/watch?v=dUizCAWHYDs

[MEDIA=facebook]206797899951405[/MEDIA]

Nafikiri Mtoa mada na uongozi wa Azam mnajua fika ni nini watz wanapenda ukija kwenye swala la masoko endapo uongozi ukikiuka hiyo formula Wajiandae kisaikoloJia.
Ila ni Good move

Namsubiri kwenye data tu.

jamaa huwa hakurupuki, kuna consultant firm moja ya huko ulaya huwa anaitumia kumfanyia utafiti wa kibiashara kabla hajawekeza katika mradi fulani.

ukiona mpaka wenyewe wameamua kutangaza, basi ujue tayari wameshajiridhidha na tayari wameshachukua tahadhari zote.

hahaha patamu hapo…vita vya panz, naamini bei ya data watapunguza bila kupenda

zile ndege zake mbona hatuzioni angani? au zinarukia zanzibar tuu?

hapo ndio kwenye mzuka… hata mimi namsubiria hapohapo.

Sisi tunachohitaji ni huduma bora tu, acha wapambane…

kwani walitangaza kuwa wanaingia kwenye biashara ya aviation?.

Huduma bora ndio hitaji la msingi kwetu watumiaji, hayo mengine watajuana wenyewe kwa wenyewe

that’s what matters.

Hongera Azam… Ila kwenye data naamini utawala huu ungependa GB moja iuezwe hata elfu kumi

Bado dstv atabakia kuwa kinala wa burudani kwa ukanda wote huu wa kusini mwa jangwa la sahara!!azam tv bado ,kinachombeba ni hiyo ligi kuu ya vodacom tu lakini tofauti na hiyo hakuna vipindi unavyoweza sema kuwa ni vya ubunifu kwenye hizo channel zake!!kuhusu kwenye sector ya mawasiliano muulize vettel/halotel alikuwa na nia gani na kilichotokea!!tena kwa sasa kuna hiyo ttcl ambayo hata kama huduma zake ni mbovu lakini lazima ikuzwe tu!!na kaa ukijua kuwa mazingira ya kodi na mambo mengine ndio yanafanya gharama za huduma/bidhaa kuwa kubwa

Vita vya panzi furaha ya kunguru

Waje tu, boat na ndege zake tutalipia kwenye mtandao wake

Hebu tufafanulie kilichompata halotel

Maneno nusu susu sio.

wewe endelea tu kujifariji…hahahaha, dstv siku hizi wanafanya PA mitaani kama wamachinga au kama makampuni ya vileo.

hapo awali walikuwa hawafanyi PA, walikiwa wanategemea kujitangaza kupitia local tvs na billboard chache pembezoni mwa barabara ya bibi titi na bagamoyo road.

ushindani toka azam umewalazimisha mpaka kushusha bei ya packages zao.

ubora wa huduma/bidhaa bila kuwa na wateja wa kutosha ni ujinga.

last week nilikuwa nasafiri kuelekea shinyanga nikitoka dar, karibia maeneo yote niliyokatiza pembezoni mwa barabara, nyumba zilikuwa zimefungwa madishi ya azam, sikuona dishi la hiyo takataka dstv.

ila halotel kwa Internet yenye kasi hawana mpinzani tz.

Upo wapi mkuu? Kwa mtazamo wangu nchi hii hakuna wenye internet yenye kasi kushinda vodacom sema tu vifurushi vyao ni bei sana.