Mmiliki wa mabasi ya zakaria ashikiliwa kwa kuwajeruhi maofisa usalama kwa bunduki

Mkuu wa mkoa wa mara amethibitisha kuwa maofisa usalama hao walifika kwenye kituo cha mafuta kinachomilikiwa na mfanya biashara huyo ambapo wawili walishuka kwenye gari na kuanza majibizano ndipo mfanya biashara huyo maarufu akachukua bastola yake na kuwajeruhi wawili, wengine waliokuwepo kwenye gari walishuka na kumpokonya bastola…ngojea tuone hili lipicha litaendaje

Labda walimkorofisha bhana

Kama kawaida kunawatakaochukua upande ili watafute sifa za kitoto.

KADA WA CCM vs POLISICCM

Watajuana wenyewe

Kwakwel wasituchoshe

Mbwa kala mbwa

Hawakuwa mapolisi mkuu wa mkoa amewatambulisha kama maofisa usalama wa taifa sijui ndio watu gani hao

Du…

Wawe Usalama wa Taifa, wawe vibaka, wawe majambazi hao hao.

Ila watajua wenyewe jinsi ya kumalizana.

Au walitaka wamteke na kumpoteza, maana hawa nao siku hizi hawaaminiki tena

Kajihami, kaogopa yasije kumtokea ya super sammy na mwandishi azory, bora nusu shari maana hadi anaruhusiwa umiliki wa silaha wahusika walidhajiridhidha na utimamu wa akili…

GIDO LAKA GIDO.

-Picha la Kihindi,TISS walikuwa wanaweka mafuta kwenye gari,Zakaria akatoka na bastola akawapiga TISS wawili kwa bastola,wakati huo huo Zakaria ana bastola wakashuka TISS wengine wakaja kumyang’anya zakaria bastola,hao TISS walioshuka walikuwa hawana bastola ndio maana hakukuwa na majibizano kati ya hao TISS walioshuka na zakaria baada ya wenzao kupigwa risasi,TISS hawana bastola huku wakishuhudia wenzao wamepigwa risasi wameshuka wakaenda kumnyang’anya Bastola zakaria,Future is exciting,are you ready?

Inakuaje uwapige wateja wako? Halafu wateja hawana silaha wakamnyang’anya silaha.Kuna maneno yamerukwa hapa

ila zac hana shabaha

Zimwi likujualo halikuli likakwisha,wanajuana hao waarabu wa pemba.

Kule JF kwwtu huu uzi ungekua una replies 200 sahiv na views 2.7k

Kuna mdaau aliletaga uzi kule JF Kuhusu dhuluma aliyofanyiwa sijui ndo huyu bilionea

Zackaria asingechukua preemptive actions angekua ameungana na super Sammy paradiso.Kudos kwake

[B][I]Leo Jumamosi Juni 30, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima ametoa ufafanuzi kuhusu tajiri huyo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Zakaria kuwa hajatwekwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Malima amesema mfanyabiashara huyo amekamatwa na maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa na kufikishwa kituo cha polisi mjini Tarime kwa ajili ya kuhojiwa, akituhumiwa kuwajeruhi kwa risasi maofisa wawili wa idara hiyo.

Amesema kabla ya tukio hilo, maofisa watano wa Usalama wa Taifa walifika katika kituo cha mafuta kinachomilikiwa na Zakaria kwa nia kujaza mafuta kwenye gari lao, “ wenzao wawili walishuka kwenye gari ghafla wakashambuliwa kwa risasi na Zakaria aliyekuwepo eneo hilo.”

"Baada ya wenzao kujeruhiwa kwa risasi, maofisa wengine walifanikiwa kumdhibiti Zakaria na kumtia mbaroni na kumkabidhi kwa polisi wanaoendelea kumhoji.”

Malima hakutaka kulizungumzia kwa undani tukio hilo lililotokea jana Juni 29, 2019 saa 2:30 usiku na kubainisha kuwa waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Tarime huku mmoja akidaiwa kuwa katika hali mbaya.

Tangu jana usiku, mji wa Tarime umekumbwa na taharuki baada ya taarifa za mfanyabiashara huyo kudaiwa kutekwa kuzagaa mitaani.[/I][/B]

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/4639504/medRes/2027933/-/4mjpu1z/-/ZACHARIA+PIC.jpg
Anaonekana kauzu??yani kweli ukajifunzie shabaha kwa maafisa??ana hatari.
Au labda ni kada wa chama cha rangi ya gari hapo nyuma ndo maana.