Mmiliki wa mabasi ya zakaria ashikiliwa kwa kuwajeruhi maofisa usalama kwa bunduki

Gideone

Senior Villager
#21
Ma ofisa wa usalama wa Taifa ndio watu gani? na wametoa wapi mamlaka ya kumkamata mtu mwenye silaha na kwenda kumkabidhi polisi..? kwaninini wasiite polisi au ata kama walimkamata jukumu la kumpeleka kituoni sio lao tutawamini vipi kama wamemfikisha kituoni je walisindikizwa na Raia wengine??
 

Demii

Senior Villager
#24
GIDO LAKA GIDO.

-Picha la Kihindi,TISS walikuwa wanaweka mafuta kwenye gari,Zakaria akatoka na bastola akawapiga TISS wawili kwa bastola,wakati huo huo Zakaria ana bastola wakashuka TISS wengine wakaja kumyang'anya zakaria bastola,hao TISS walioshuka walikuwa hawana bastola ndio maana hakukuwa na majibizano kati ya hao TISS walioshuka na zakaria baada ya wenzao kupigwa risasi,TISS hawana bastola huku wakishuhudia wenzao wamepigwa risasi wameshuka wakaenda kumnyang'anya Bastola zakaria,Future is exciting,are you ready?
From nowhere tu mtu aanze kufurumusha risasi?
 

bababikko

Senior Villager
#27
Leo Jumamosi Juni 30, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima ametoa ufafanuzi kuhusu tajiri huyo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Zakaria kuwa hajatwekwa.


Akizungumza na waandishi wa habari Malima amesema mfanyabiashara huyo amekamatwa na maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa na kufikishwa kituo cha polisi mjini Tarime kwa ajili ya kuhojiwa, akituhumiwa kuwajeruhi kwa risasi maofisa wawili wa idara hiyo.


Amesema kabla ya tukio hilo, maofisa watano wa Usalama wa Taifa walifika katika kituo cha mafuta kinachomilikiwa na Zakaria kwa nia kujaza mafuta kwenye gari lao, “ wenzao wawili walishuka kwenye gari ghafla wakashambuliwa kwa risasi na Zakaria aliyekuwepo eneo hilo.”


"Baada ya wenzao kujeruhiwa kwa risasi, maofisa wengine walifanikiwa kumdhibiti Zakaria na kumtia mbaroni na kumkabidhi kwa polisi wanaoendelea kumhoji.”


Malima hakutaka kulizungumzia kwa undani tukio hilo lililotokea jana Juni 29, 2019 saa 2:30 usiku na kubainisha kuwa waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Tarime huku mmoja akidaiwa kuwa katika hali mbaya.


Tangu jana usiku, mji wa Tarime umekumbwa na taharuki baada ya taarifa za mfanyabiashara huyo kudaiwa kutekwa kuzagaa mitaani.
Huyu malima anapindisha kama ilivyotokea morogoro aliponyanya dodo za changudoa pale nashera hotel akajikuta kasinzia demu keshaondoka na madola ya kutosha
 

Waso

Senior Villager
#30
Jiwe limeumbuka na kashoga kake kanakosimamia mauaji ya wanaoenda kinyume nae. Mwaka huu nundu itahamia matakoni shenzi zake na ushamba wake.
 

Muthewo

Senior Villager
#31
Inakuwaje muuza mafuta awapige risasi wateja???..............kuna taaruki kutokana na taarifa za kutekwa kwa muuza mafuta!!!!....na wanunuzi wa mafuta ni usalama wa taifa!!!!!......
 
#32
Hadi sasa sijapata taarifa ya kuamini, hivi inakuaje mteja anapigwa risasa mayb only in Tanzania. Kuna mengi yamejificha nyuma ya pazia.
 

Tindo

Village Elder
#35
Kama kawaida kunawatakaochukua upande ili watafute sifa za kitoto.
Nani atachukua upande kwa mambo ya kipuuzi? Sana sana wenye akili wanajiuliza inakuwaje suala linalopaswa kutolewa maelezo na jeshi la polisi linatolewa maelezo na RC? Wakati mwingine yanafanyika mambo yenye nia ovu na kusababisha watu kuhoji weledi wa wenye mamlaka. Sasa watu wakionyesha walakini kwenye huo upuuzi mnasema watu wanatake side.
 

chemical Ali

Senior Villager
#37
Nani atachukua upande kwa mambo ya kipuuzi? Sana sana wenye akili wanajiuliza inakuwaje suala linalopaswa kutolewa maelezo na jeshi la polisi linatolewa maelezo na RC? Wakati mwingine yanafanyika mambo yenye nia ovu na kusababisha watu kuhoji weledi wa wenye mamlaka. Sasa watu wakionyesha walakini kwenye huo upuuzi mnasema watu wanatake side.
RC ndio mwenyekiti wa kamati na usalama wa mkoa sidhani kama anakosa kutoa taarifa
 

Tindo

Village Elder
#38
RC ndio mwenyekiti wa kamati na usalama wa mkoa sidhani kama anakosa kutoa taarifa
Ili nikuelewe vizuri kwa huu utetezi wako, kuna matukio mengi sana ya jinai huwa yanatokea hapo Mara, mkuu wa mkoa anakuwa wapi kutolea maelezo? Au hicho cheo chake kinachagua cha kutolea ufafanuzi? Hicho cheo cha mwenyekiti wa usalama wa mkoa ni kuingiza siasa chafu kwenye taaluma. Na ni dhahiri hata kama huyo Zacharia naye ni mchafu, lakini hili linalofanyika nayo ni muendelezo huohuo wa uchafu.
 
#40
Hawakuwa mapolisi mkuu wa mkoa amewatambulisha kama maofisa usalama wa taifa sijui ndio watu gani hao

Mkuu amewatambulisha kama maofisa usalama wa taifa au maofisa wa usalama? Maana kuna vitu viwili tofauti hapo!

Ila yote tisa, kumi hao wote ni watoto wa baba mmoja, tuchukue jembe tukalime. Wakipatana tutaenda kuvuna tupate grease
 

Top