Mimi Lizaboni kwa hili la kufungiwa jf sikubaliani nalo simuungi tena mkono magufuli

Nimekipigania chama cha ccm mno pale jf ndani na nje ya ccm

Nimetukwanwa,nimesakamwa,kisa natetea ccm mengi sikua nayaunga mkono ila nikaona nivumilie tu yatapita ila sasa hali ni tete

Sikua najua kama tutafikia hapa tulipo nimekua miongoni mwa watu walowaita kina nape wasaliti ila nimejifunza kukaa kimya na uvumilivu umenishinda tangia kupotea kwa jf nimeamua kuanzia leo sitomuunga tena mkono magufuli

Ndugu zangu kama niliwakosea mnisamehe hususani kule.jamiiforums mimi ni binadamu kama nyie

CCM tumeijenga kwa maumivu, uchungu na hoja nzito tangia inaandamwa na lawama za ufisadi

Magufuli nimekupigania mtandaoni mpaka nikatumia mpaka na IDs fake na account fake mpaka facebook, jf na insta kwa sasa imetosha

Badala ya kuona mwanga tunazidi kuelekea gizani

Kuanzia leo sitomuunga mkono tena magufuli kwa hili la jamiiforums na mipango mibaya na tcra dhidi ya mitandao naogopa historia kunihukumu kwa hili simuungi mkono raisi wangu dk john pombe magufuli
cc @mitochini @msagasumu

Sio lizaboni ninayemfahamu.

Hili la JF limeniuma…natamani kuhama Tz

Nahisi kama wamehack account yako, yaani siamini kama yule lizaboni ninayemjua mie

bado jinga lao…

Ha:):):):)hahaha

Pole sana…

Its too late…

Cc: @Mahondaw

imekuaje mkahama na ID zenu mimi mbona nimelazimika kutengeneza mpya mkuu

Duh!

Mbona inawezekana kuingia kwa id yako ya zamani, mie sijapata shida

Huyu sio Lizabon huyu.

Tahadharini watu watakuja na ID za watu humu.

Muwe makini huko Inbox.

Kama ni wewe kweli hongera maana ule ukimya wako ulikuwa sio wa kawaida.

Kweli kabisa mkuu

Nashukuru nawe kwa kulitambua hilo.

Mwingine atakuja akisema yeye ni Nyani Ngabu kumbe sio, watu wawe makini humu.

Huyu sio Lizaboni, ni mtu mwingine tu kajiunga kwa ID ya Lizaboni

Mwandiko wenyewe unajieleza kuwa sio mwenyewe, kwa mnaofahamu mwandiko wa Lizaboni mtathibitisha

Mimi binafsi nilikuwa natamani watu wote waje na ID zao za JF lakini ndio hivyo huwezi kumpangia mtu maamuzi yake

Yaah, lilikuwa ni jambo jema hasa katika muendelezo wa kufahamiana.

Huyu sio Lizaboni acheni kutumia IDs za watu!

Pia kuja na ID tofauti na ile ya mwanzo sio vibaya kwa kuendeleza kutunza privacy ila hili la kuja kwa ID ya mtu sio vizuri aisee

sema humuungi sababu wamekata ile buku saba.

Aahhha haa