Mchuzi wa maharage ya aina tatu

Sky Eclat

Village Elder
#1
Mahitaji:
Maharage cheupe gram 250
Maharage ya jesca gram 250
Maharage ya selian 94 gram 250
Kitunguu kikubwa kimoja kilichokatwa
Gramu masala kijiko kimoja cha chai
Thomu ya kitunguu saumu
Nyanya kubwa 2 zilizokatwa
Chumvi kijiko cha chai kimoja
Sukari 1/2 kijiko cha chai
Pilipili kichaa 1
Gililian iliyokatwa viapande vidogo dogo
Mafuta 200 mills (huwa ninatumia olive oil)
Tui la nazi (ukipenda)

1530544095201.png

Jinsi ya kupika:
Chemsha maharage mpaka yaive lakini usiyaache yalegee saana,
Kaanga kitunguu mpaka kiwe hudhurungi,
Ongeza Thomu ya kitungu saumu
Changanya nyanya, weka garamu masala na pilipili,
Weka maharage yako kwenya mchanganyiko huu pamoja na chumvi na sukari
Acha vichemke kwa dakika 10, weka giligiliani na (tui la la nazi ukipenda)
1530543946704.png
 

Top