Mchango wenu kuhusu hili wakuu

Wakuu habarini ,nna mtaji wa Tsh million 15,mm ni mpenz wa technology na ningependa kuwekeza fedha hizi katika moja ya biashara hizi mbili, moja ni kuuza simu na laptop na bidhaa nyingine za ki electronic , idea nyingine kwa kuwa ni mpenz wa video games na nimezicheza miaka nenda rudi nawaza kufungua centre ya michezo ya video yenye vifaa vya kisasa kama ps 4 xbox na flat screen na computer znr. Naomba ushaur wako je ni biashara ipi itafaa kulingana na mtaji wangu na hali ya ss iv . Nko mkoa wa Dar es salaam.

Uza simu na vifaa vyake
Na laptop

Mkuu naomba niende nje ya eneo unalopenda wewe, kama ukiweza ukatoa Million 5 ukaenda Manyara ukaingia kwenye biashara ya kununua alzeti na kukamua mafuta, hakika usingeweza kujutia uamuzi huo. Endapo utahitaji maelezo zaidi niulize nitakueleza kadri nitakavyoweza