Mbunge Joseph Mbilinyi (Sugu) kuiburuza Basata mahakamani kutokana na kuufungia wimbo wake

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kwa jina la Sugu, amesema amewaandaa mawakili wake 6 tayari kwa kuwapeleka Basata mahakamani kutokana na kuufungia wimbo wake unaoitwa Mfungwa na 219

Atakuwa amefanya uamuzi wa busara wa kuiburuza mahakamani Basata ili ikaeleze sababu za kuufungia wimbo wake

Hata Mimi nimejaribu kuusikiliza wimbo huo, sijaona sehemu yoyote ya uchochezi, kama inavyodaiwa na Basata

Sugu ameimba ukweli mtupu katika wimbo wake huo kuwa yeye hakufungwa kwa kosa la jinai Bali alifungwa kisiasa

Je uongo wake au uchochezi hapo ni upi??

Katika wimbo huo pia ameeleza kuhusiana na kupigwa risasi yule mwanafunzi Akwilina aliyekuwa kwenye daladala na kuuawa, na baadaye DPP akafunga faili lake kwa madai kuwa wameshindwa kumbaini Muuaji!

Je katika hill nalo uongo wa Sugu au uchochezi wake ni upi??

Hii Tanzania kwa bahati mbaya sana, taasisi karibu zote za kiserikali, zinafanya kazi kwa ajili ya kumfurahisha Bosi wao Magufuli!

Vyombo hivyo vya dola havifanyi tena kazi kwa weledi na taaluma inavyowataka wafanye, kama vilivyokuwa vikifanya kazi awali.

Ee Mwenyezi Mungu, turehemu waja wako waTZ, kutokana na dhahama hii inayotukabili ya utawala wa kidhalimu wa huyu mtu anayeitwa Magufuli

Amri kutoka juu ndiyo imepekekea BASATA kuufungia mwimbo wa rais wa Mbeya

Nchi hii hata mwendawazimu anaweza kuwa rais wa nchi, uongozi wa awamu hii unadhihirisha hili

Aisee kweli kabisa…

Nami nina mashaka kama kweli huyu tuliye naye hivi sasa kama huko upstairs yupo sawa kweli

!
!
Kujipendekeza Tu Kwa Basata.

Amri kutoka kwa Magufool.

Ni afadhali kuwa na jeshi la kondoo linaloongozwa na Simba, kuliko jeshi la simba linaloongozwa na kondoo…
Hivyo sishangazwi na yanayojiri

Bora aisee

Sasa hao BASATA wataenda elezea hiyo kitu kwenye mahakama

Kwa kuwa kama ni uchochezi basi DPP wa Tanzania ndiye angepaswa awe mchochezi no 1 nchini. Kwa kuwa wakati Kamanda wa Polisi kwenye kanda maalum ya Dar, Bwana Athumani Mambosasa alitueleza kuwa risasi iliyomwua Akwilina ilifyatuliwa na mmoja wa askari wake na akaendelea kueleza kuwa wamewaweka ndani askari wake 6 kwa uchunguzi

Lakini cha ajabu baada ya siku chache tunamsikia DPP akisema kuwa wamefunga faili la Akwilina kwa kuwa wameshindwa kumbaini Muuaji!

Hivi hali hiyo inatoa picha gani kwa familia ya Akwilina na Umma wa watanzania kwa ujumla?

Ni dhahiri kuwa picha inayopatikana hapo bi kuwa Polisi wa TZ anaruhusiwa kuua raia wa nchi hii bila kuchukuliwa hatua yoyote!

Sidhani kama Rais amewaagiza BASATA kufungia nyimbo. Tuacheni kumtwisha Mzigo raisi,
Hao basata wamechemka tu kama wale wazee wa rula na samaki

Lengo lao lilikuwa kumfurahisha ndugu Jiwe

Kama watakua wanafanya kazi hivi basi tuna safari ndefu sana!!! watu wanatakiwa wafanye kazi kwa utashi wao hakuna jingine

Hii nchi ishaharibika sana…

Imagine Jeshi la Polisi linazuia mikutano ya hadhara ya wapinzani, hapo hapo wanaruhusu ya CCM iendelee kama kawaida

Kisa kwa kuwa Bwana Mkubwa kapiga marufuku mikutano ya kisiasa hadi mwaka 2020!

Ni kwanini hawatumii weledi na kuona, je sheria ndivyo inavyotaka hivyo au ni matakwa ya Mr Jiwe pekee??

Ni ujinga ule ule.
V Money akivaa kichupi kosa,Rihhana akicheza uchi sawa
Emmeniem akimpasha Trump sawa Roma akimpasha Uchwara kosa.
Kila moja anafurama kumfurahisha mshamba wa Chatto

Nimejaribu kuusikiliza wimbo huo wa Sugu sijaona sehemu yoyote ambayo ni ya uchochezi kama wanavyodai hao BASATA

Mathalani kuna sehemu ameviuliza vyombo vya usalama kuwa mnataka kunishoot kama mlivyomfanyia Lissu?

Sijaona uchochezi kwa kauli hiyo

Hivi kama siyo vyombo vya usalama ndivyo ilivyomshoot Lissu, ngoja niwaulize maswali machache tu vyombo hivyo vya Usalama

  1. Ni kwanini huu ni mwezi wa 9 hakuna hata mtu mmoja ambaye amekamatwa kuhusiana na tukio hilo??

  2. Kama vyombo vyetu vya usalama vya ndani vimeshindwa kuwapata watu waliohusika na tukio hilo, je ni kwanini linapotolewa pendekezo la kuvileta by omen vya nje vije visaidie kufanya uchunguzi, vyombo hivyo vya ndani vinakataa??

  3. Ni kwanini CCTV Camera zilizilokuwa kwa Mheshimiwa Kalemani zilinyofolewa Mara tu baada ya tukio lile??

  4. Hivi ni kwanini Waziri wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba na IGP Sirro hawajiuzulu kutokana na tukio hilo la kupigwa risasi mchana kweupe tena kwenye makazi ya viongozi wa Kitaifa??

Nitashukuru iwapo vyombo husika vitajitokeza na kunijibia maswali yangu hayo

Time will tell…

Cc: @Mahondaw

Yajayo ni mengi

Yajayo ni mengi, ila tunamwomba Mungu wetu atuepushe na balaa hiyo inayotikabili kama Taifa

Amri Kutoka juu ndiyo hiyo pia itaamrisha mahakama kutupilia mbali kesi yake.