Mbona hamtupi mrejesho wa hiyo Forum mpya "Bongoforums"?

Nimechungulia huko nimewaona wakina @pyepyepye @Allen Kilewella @gemmanuel265 @Washawashatz

Binafsi haijanivuta ngoja nitulie hapa.

Mkuu Huko Bado hakueleweki

Kukoje kwani

Siwezi kujisajili hata kwa bahati mbaya forum mpya za kibongo na kama ningehitaji kuendelea kuwa bongo ningeenda mwanahalisi forum ambayo ni ya kitambo hiyo forum yao hiyo imekaa kimkakati

Mkuu hiyo forum imedoda kishenzi, nadhani ni post moja tu ina page 2. Imechakaa kabla haijanza. Na trend ilivyo ni kama member wa jf original wamefahamu hii jf ya huku ukimbizini. Sidhani kama itachukua zaidi ya mwezi kabla member wote wa jf Tz hawahaingia humu. Unaweza dhibiti mbuzi sio binadamu kwa dunia ya sasa kama familia yako. Kuna forum nyingine inaitwa tuzungumzeforum. Hiyo ndio janga kabisa. Nadhani mods huko ni jenist mhagamaaaa na slowslow. Hiyo iko kama uji wa baridi usio na sukari.

Kule msiende!!

Lile ni tego la FISIEM na LUMUMBA!! Kuwanasa wadau wote wa kujenga hoja kwa maendeleo ya taifa.

kule kuna jamaa yangu kaniambia alijisajil kwa jina fake akashangaa mtu anamquote we “jina lake halisi” Hujambo? alitoka nduki break ya kwanza KT.

:D:D:D:D

Nitakuwa wa mwisho kuiamini kama haijaanzishwa na Lumumba

Halafu shida sio kupata forums mpya tatizo ni madini yaliyomo JamiiForums

:D:D Simpatii picha alivyoduwaa

[ATTACH=full]178918[/ATTACH]

HUKO SIENDI…maana wasiojulikana watakuwa wengi…

:D:D:D:D…sio muda mrefu uliopita kuna nyang’au humu zilijaribu kuanzisha forums zao wakiiga hii KT, matokeo wanayafahamu wenyewe…walirudi huku mmoja baada ya mwingine kwa unyenyekevu mkubwa na wakatulia

Kwa wasiojua hizi forum mpya zinazoanzishwa kwa jina linaloshabihiana na jamii forum zipo kimtego wanajua wengi baada ya jukwaa letu pendwa kuwa offline member wengi wataenda kujisajili mwisho wa Siku wanadakwa wote…

mbulaaaah siend tena

Kwahizi comments nilizo zisoma, tayari nimejiridhisha kwamba sihitaji hata kuijua hiyo Bongo forums.
Ebu ngoja niendelee kuwa mtulivu hapa KT

Mwaka huu zitaanzishww forums nyingi sana! Na tutaona mengi kweli kweli

ile itakufa kabla haijanoga