Masiku yanayo haramishwa kufunga na yanayo chukiza

#1
Kwanza: Masiku yanayo haramishwa
1. Ni haramu kufunga siku za idd Mbili Amepokeya Abuu Hurayra t Kwamba Mtume (saw) (Amekataza kufunga siku mbili: Siku ya Adh’ha na Siku ya Fitr) [Imepokewa na Muslim.]

2. Ni haramu kufunga siku za Tashriiq, nazo nisiku tatu baada ya iddul’Adh’ha, Amesema Mtume (saw) (siku za tashriiq ni siku za kula na kunywa) [Imepokewa na Muslim.]

Lakini inafaa kwa mahujaji kufunga ikiwa hija yake ilikuwa ni kwania ya Tamattu na Qiran na asipate mnyama wa kuchinja kwa neno lake Mwenyezi Mungu (Basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya umra kisha ndio akahiji, basi achinje mnyama aliye mwepesi kumpata.na asiye pata afunge siku tatu katika hija na siku saba mtakapo rudi) [Al-baqara: 196]

3. Niharamu kufunga Siku ya shaka, nayo nisiku ya thalathini ya mwezi wa Shabani, ikiwa usikuwake ni usiku wa mawingu au vumbi lakutowezekana kuonekana Mwezi, Kwa neno lake Ammaar t (Mwenye kufunga siku ya Shaka hakika amemuasi babake Qaasim (saw) [Imepokewa na Tirmidhi na akasema ni hadithi nzuri swahihi.]

Pili: Masiku Ambayo ni makruhu kufunga
1. Ni makuruhu kupwekesha mwezi wa Rajabu kwa kufunga, kwa sababu alama za watu wa jahiliya ni kutukuza mwezi wa Rajab, na katika kuhusisha kuufunga ni katika kuhuisha alama zao

2. Ni makuruhu kufunga siku ya ijumaa kwa kukatazwa kufanya hivyo, Amepokeya Abuu Hureyra t Amesema: Amesema Mtume (saw) ( Asifunge mmoja wenu siku ya ijumaa ila afunge siku kabla yake au siku baada yake) [ Imepokewa na Muslim.]

Isipokuwa ikisadifu ada ya mtu basi atafunga wala si makuruhu kwake kufunga.

3. Ni Makruhu kuunganisha Saumu, nao ni mtu kufunga siku mbili mfululizo bila ya kufunguwa, kwa sababu Mtume alikataza kuunganisha Saumu, Amepokeya Abdullah bin Umar t Amesema Amekataza Mtume (saw) Kuunganisha wakasema kumuuliza wewe waunganisha akasema (mimi si kama nyinyi mimi nalishwa na kunyeshwa) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

https://www.al-feqh.com/sw/saumu-funga-za-sunnah
 

Top