Masharti ya kufanya Swala iwe sahihi

#1
Kwanza: kuingia wakati
Swala ya faradhi ina wakati ambao haiswihi kabla yake, wala baada yake isipokuwa kwa dharura. Asema Mwenyezi Mungu aliyetukuka: { Hakika Swala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalum} [4: 103],

yaani imefaradhiwa katika vipindi maalumu.

Nyakati za Swala ni: .

1. Wakati wa Alfajiri:
Ni kuanzia kutoka alfajiri ya kweli, nao ni ule weupe unaokuwa kwenye pambizo upande wa Mashariki, mpaka kuchomoza jua.
2. Wakati wa Adhuhuri:
Ni kuanzia kupinduka jua mpaka kivuli cha kitu kiwe mfano wake, baada ya kile kivuli cha kupinduka jua. Hivyo ni kwamba jua likichomoza kitu kinachosimama huwa na kivuli upande wa magharibi, kisha kivuli hiko huenda kikipungua kila jua likipanda mpaka kivuli kisimame. Kisha kivuli kinaanza kuongezeka, na ongezeko hili lianzapo hua ndio wakati wa kupinduka.
3. Wakati wa Alasiri:
Ni kuanzia wakati wa Adhuhuri kuisha mpaka kivuli cha kitu kiwe ni mara mbili yake baada ya kivuli cha kupinduka jua.
4. Wakati wa Magharibi:
Ni kuanzia jua linapozama mpaka yapotee mawingu mekundu, nayo ni ule mwangaza mwekundu unaokuwa kwenye pembe za mbingu pale jua linapozama.
5. Wakati wa Isha:
Ni kuanzia kipindi cha Magharibi mpaka nusu ya usiku, kwa neno lake ﷺ: (Wakati wa Swala ya Isha ni mpaka usiku wa kati) [ Imepokewa na Muslim.].
Na katika zama hizi, inawezekana kujua nyakati za Swala kwa urahisi kwa njia ya kuweka jaduali za kujulisha nyakati.
https://www.al-feqh.com/sw/masharti-ya-kufanya-swala-iwe-sahihi
 

Top