Mashabiki hao waliamua kuchukua uamuzi wa kuchora picha ya rafiki yao ambaye wangeambatana naye kwenda Urusi kushuhudia Michuano ya kombe la Dunia ambapo timu yao ya Taifa ni miongoni mwa washirikii wa Kombe la Dunia.
Lakini rafiki yao hakuweza kwenda Urusi baada ya kukatazwa na mke wake na akaamua kutii amri.
Jana Mexico imecheza mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Mabingwa watetezi Ujerumani ambapo Mexico iliibuka na ushindi wa bao 1 kwa nunge
Kweli mkuu, halafu hawa rafiki zake wameonesha upendo wa hali ya juu sana hadi wakaamua wawe na picha kama kielelezo cha uwepo wa rafiki yao, Ona pale hadi wanaiweka picha kwenye kochi kama mtu kabisa
Wenzetu wakipendana ni upendo wa kweli sio kama wengine
Wengi wetu hatuna subira na tunapenda kutosikia mawazo ya wanawake ambayo ukiongea naye vizuri mnaamua vizuri kwa pamoja.
Huyo wa kuzaba vibao sidhani kama alifanya vyema, angeondoka tu bila kumpiga mkewe ingekuwa bora zaidi maana hata kama wangekuja kununiana baadae jambo lingekuwa na kawaida tu