Mapishi ya maharage ya nazi

Vipimo

Maharage - 3 Vikombe

Tui la nazi zito - 1½ kikombe

Kitunguu - 1 kikubwa

Nyanya - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi - 3

Chumvi - Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

[ol]
[li] Chemsha maharage hadi yawive haswa yalainike [/li][li]Katakata kitunguu, nyanya, na thomu kisha miminia katika maharage [/li][li]Tia tui la nazi na subiri kidogo lichemkie humo [/li][li]Weka chumvi kiasi na koroga iliuonje, kisha tupia pilipili mbichi na kisha funika kwa muda kadhaa hadi libaki rojo rojo [/li][li]Baada ya hapo pakua na tayari kuliwa[/li][/ol]
[ATTACH=full]180046[/ATTACH]

Sky Eclat, hapo kwenye maharage aka ndondo ndiyo chakula changu ati, nikipata wali na ndondo roho yangu inasuuzika…

napenda lkn duuh kukuna nazi shughuli. @Sky Eclat kwani lazm nazi ya kukuna? au hat ya pakt inafaa

Ya pakiti inafaa pia

swadakta!