Mapishi ya maharage ya nazi

Sky Eclat

Village Elder
#1
Vipimo

Maharage - 3 Vikombe

Tui la nazi zito - 1½ kikombe

Kitunguu - 1 kikubwa

Nyanya - 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi - 3

Chumvi - Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha maharage hadi yawive haswa yalainike
  2. Katakata kitunguu, nyanya, na thomu kisha miminia katika maharage
  3. Tia tui la nazi na subiri kidogo lichemkie humo
  4. Weka chumvi kiasi na koroga iliuonje, kisha tupia pilipili mbichi na kisha funika kwa muda kadhaa hadi libaki rojo rojo
  5. Baada ya hapo pakua na tayari kuliwa
1530096782085.png
 

Top