Mapishi ya kalimati

Sky Eclat

Village Elder
#1
Mapishi ya Kalimati
Mahitaji:
1. Unga nusu kilo
2. Sukari robo kilo
3. Hiliki ya kusaga vijiko viwili (2) vidogo
4. Vanila ya maji vifuniko viwili (2)
5. Mafuta ya kupikia
6. Nazi moja (1)
7. Hamira kijiko kidogo kimoja (1)

Jinsi ya Kupika:

Kuna nazi na uichuje vizuri, chukua chombo chako kisafi cha kuumulia kalimati zako na uweke unga wako, weka hamira yote, weka hiliki yote, weka sukari na vanilla kisha uweke tui bubu la nazi (la kwanza) kiasi na uanze kuchanganya. Changanya unga na mkono mpaka ulainike. Hakikisha ukiweka tui lako usiweke jingi lisije likawa jepesi sana ukashindwa kuchota saa ya kuchoma. Acha unga mpaka uumuke.

Unga ukishaumuka waka mafuta jikoni na yakishapata moto anza kuchoma kalimati kwa saizi utakayo hadi zitakapokuwa rangi ya kahawia (brown) zitoe motoni.
1530096469191.png
 

Top