Magufuli na ccm someni hapa: Madhara ya kuamini kuwa propaganda inafanya kazi wakati wote

It is a long reading; but for the sake of our country please read.

Kuna hadithi nilipata kuisoma zamani. Bwana mmoja aliependa kudanganya wenzake aliamua siku moja kupita mtaani kuwandanganya wanakijiji wenzake. “Jamani kesho mchana kwa jumbe kutakuwa na karamu. Jumbe atachinja ng’ombe wawili na kutakuwa na pilau na wali na vinywaji kedekede”. Akarudia kuwaambia uzushi wake huo watu wengi. Ila alikuwa mwangalifu; HAKUWAAMBIA WATU WENYE NAFASI YA KUKUTANA NA JUMBE au kuwa na namna ya ku-verify hiyo taarifa bandia.

Kesho yake bwana huyu akakaa barazani kwake kuona watu wangapi wataamini uzushi wake ili awacheke. Akapita mtu wa kwanza kuelekea kwa jumbe akiwa amevalia vizuri kweli kweli; mtu huyu akamuuliza: " wewe huendi kwenye karamu kwa jumbe ili hali ulitutaarifu hizo habari wewe mwenyewe?" Mzushi akajibu; “muda bado, nami naja”. Akapita wa pili, wa tatu, na wa nne. Akiulizwa swali lile lile kama alivyoulizwa na mtu wa kwanza, na mzushi akijibu vile vile. Idadi ya watu waliodanganywa ilipoongezeka mzushi akaanza kujiuliza; “ni kweli nilizusha hili jambo la karamu, lakini mbona watu wanaokwenda kwa jumbe ni wengi kuliko niliowandanganya mimi? Isije ikawa kwa jumbe kuna karamu kweli na mimi nikapitwa nimekaa hapa hapa!”

Bwana mzushi akaingia ndani, akajikwatua kweli kweli nae akajiunga kwenda kwa jumbe. Kufika akakuta watu wengi kweli kweli ila jumbe hakuwepo (kumbe siku ile jumbe alikuwa safari mbali kidogo kwa shughuli nyingine). Kurudi nyumbani kwake, “hamadi” uwanja umejaa watu. Jumbe kuuliza kulikoni, akaambiwa wamekuja kwenye karamu. Jumbe akashangaa kudaiwa karamu asiyoiandaa. Mzushi akaumbuka!

TURUDI KWENYE HALI HALISI NCHINI
Uongo mnaouzusha nyie ccm utawagahrimu wenyewe. Tatizo ni kuwa mmeanza kuuamini uongo wenu wenyewe hadi kufikia kuwafanyia ukatili watu wasiotaka kujiunga kwenye mkumbo wa kukubali uongo wenu. Mlipoanza mlijua mnadanganya (Marehemu Horace Kolimba, Katibu Mkuu wenu wenyewe enzi ya awamu ya pili alipata kuwaambia hivi: “ccm imepoteza mwelekeo”. Na hiyo ilikuwa miaka ya 90. Hamkumsikiliza; mkaendelea kuamini uongo wenu. “Tanzania ni nchi ya kupigiwa mfano, Tanzania kisiwa cha amani, Tanzania inaonewa wivu kwa maendeleo yake, tuna viongozi mahiri kweli kweli etc, etc, etc”. Je, hali halisi inaakisi hayo mnayoyasema"

Leo hii mnayoyazusha ni mambo mengi mno - na kwa bahati mbaya mnaendelea kuuamini uzushi wenu wenyewe. naomba nitoe mfano:

Leo hii mnatuambia kuwa mnataka Tanzania ya viwanda na kuwa “tunataka tuzalishe nguo nyingi ili tuwapelekee wazungu mitumba baada ya sisi kuzivaa zikiwa mpya”. Wazalishaji wakubwa wa pamba duniani kwa takwimu za 2017 ni (in that order); - (vipimo ni katika metric tonnes)

[INDENT=2]1 China 6,532[/INDENT]
[INDENT=2]2 India 6,423[/INDENT]
[INDENT=2]3 United States 3,553[/INDENT]
[INDENT=2]4 Pakistan 2,308[/INDENT]
Lakini wazalishaji wakubwa wa nguo (textile) duniani kwa takwimu hizo hizo ni China, Bangladesh, India, Vietnam, Ethiopia, Indonesia, Sri Lanka na Phillipines.
Mmmeshawahi kujiuliza ni kwa nini hali ipo hivyo? Mmmeshawahi kujiuliza hivyo “viwanda” mnavyowaambia kina Mnyeti watoe amri hadharani kwa wakuu wa wilaya mikoani mwao wahakikishe ndani ya mwaka vinaanzishwa viwanda kadhaa kwa kila wilaya:
[INDENT=2]Vitazalisha nini?[/INDENT]
[INDENT=2]Kwa ajili ya nani?[/INDENT]
[INDENT=2]Mbadala wa hizo bidhaa ni nini? (competing goods - quality and price of imported ones)[/INDENT]
[INDENT=2]Uwezo wa walengwa kununua hizo bidhaa zitakazozalishwa (demand) ni upi?[/INDENT]
[INDENT=2]Malighafi ya kutengenezea hizo bidhaa zitatoka wapi?[/INDENT]
[INDENT=2]Skilled labour ya kuendesha hivyo viwanda (in production, marketing, financial management and other supporting staff) watatoka wapi?[/INDENT]
[INDENT=2]Mtaji (kwa maana ya capital expenditure and working capital) utapatikana wapi?[/INDENT]
[INDENT=2]etc, etc, etc[/INDENT]
[INDENT=2][/INDENT]
Mmeshawahi kujiuliza haya maswali au ndio mnaamini uzushi wa " tunataka Tanzania ya viwanda"? Kama jumbe alivyomuumbua yule mzushi, nanyi mkiendelea hivi jiandaeni kuumbuka. Na muda si mrefu ujao kuumbuka kwenu kutakuwa dhahiri.

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE

Mkuu,hawa wana CCM ni watu wa ajabu sana. Kuumbuka wameshaumbuka mara nyingi sana na kitambo kirefu,na wataendelea kuumbuka mpaka kifo cha CCM.
Leo wabunge wa CCM wamesisitiziwa ati waishauri/waisimamie serikali na wakati huo huo wakipiganie/kukilinda chama chao.Nimejiuliza sana uwezekano wa kusonga mbele kimaendeleo kwa utaratibu huu,nimegundua haiwezekani.

Hiyo statement tu inajicontradict

Wakati huo huo uisimsmie serikali iliyoko madarakani, wakati huo huo ukilinde Chama chako kisianguke…

Ifahamike pia kuwa Serikali iliyoko madarakani inaongozwa na Chama hicho hicho cha CCM ambacho wabunge wa CCM wamelishwa “amini” kuwa hawapaswi kukisaliti!

Ciciemu na bichwa ni takataka had I watu wa kabila lake wamemchoka simuizi wanmwita kichaa

MCC walivyo wavivu kusoma sijui kama wataisoma post yako yote!

Kuweni na imani nao tuu. Wanatujengea vi…wonder. Haaaaaahaaaaaa

!
!
Maamae Hawaelewi

Bora nchi iuzwe nipewe changu nisepe

Kutegemea Tanzania ya viwanda chini ya utawala wa kikaburu toka ccm ni kupotezeana muda tu

Tumeshauzwa, ndio maana leo tumepanga Kenya in Kundambanda’s voice (RIP). Huyu mmakonde aliwahi kututabiria haya maswahibu

siku watayobadili hicho kibwagizo cha “tanzania ya viwanda” hutaamini kama ni wao, watakuja na msemo mpya na hawatakunbuka tena msemo wa zamani. wako kama ma zombie flani hivi, yaani kila kiongozi anayehojiwa kwenye media anajitahidi kuungaunga maneno mwishoni ionekane anachokifanya kitachangia “kuelekea tanzania ya viwanda” yaani hadi viongozi wa jeshi wameiga huo upuuzi!! shame

Ni afadhali kuwa na jeshi la kondoo linaloongozwa na Simba, kuliko jeshi la simba linaloongozwa na kondoo

[QUOTE="
MWENYE MASIKIO NA ASIKIE[/QUOTE]

Mkuu umeua kabisa umepita mule mule.

Walianzaga na “hapa kazi tu” siku hizi hata hawataki kuisikia hiyo kauli

Mkuu umeongea nondo balaa

Yanasikitisha sana…

Cc: @Mahondaw

Ngumu kumeza

Hawawezi kusema tena “Hapa Kazi tu” wakati wanachofanya ni “USANII NA WIZI TU”

Mwisho wa uongo pia huwa ni aibu.

Kabur mweusi.