Kwanini ili kuwa mlinzi wa Papa huko Vatican ni lazima uwe raia wa Uswiss?

[ATTACH=full]180434[/ATTACH]
Nimekuwa nikiwaona walinzi wa Papa wakiwa wamevalia mavazi ya aina yake, kuna wakati nikataka kujua huwa wanapatikanaje, ndipo nilipogundua kuwa ni lazima uwe na sifa fulani ili kuwa mlinzi wa Papa, katika sifa hizo, sina shaka kuhusu hizi sifa zingine kama: (1) Lazima uwe Mkatoliki; (2) Lazima uwe haujaoa; (3) Lazima uwe na umri wa kati ya miaka 19-30; na (4) Lazima uwe na urefu wa angalau sentimenta 175.

Lakini najiuliza kwanini ni lazima uwe raia wa Uswiss?..

wana sifa ya kupigana kufa na kupona, miaka ya 1570 katika uongozi wa king Clement kwenye vita ya roman empire wanajesh weng hata wa roma wenyewe walisanda jamaa wao wakapigana mpk mwisho wakaweza kumwokoa mfalme kutoka kwa maadui huku wenzao takriban 190 wakipoteza maisha katika kumpigania mkuu wao, ikawapa heshma kuanzia mwaka 1816 mpk leo sio papa tu ila vatcan yote inalindwa na wa Swiss hasa sehem nyeti ila mafunzo wanapata kutoka kwa wataliano wenyewe.

Aisee!..

Hata viwanda vya hela viko Uswisi:rolleyes::rolleyes:

Hizo sifa ni kwa jinsi yeyote au

Na kwa sababu tukio hilo lilitokea May 6, ili kuwawenzi wapiganaji hao, walinzi wapya huapishwa kila tarehe 6/5 ya kila mwaka.

Wanaume tu, wao wanasema mpango wa kuwa na walinzi wanawake upo ila haujaanza kufanya kazi.

huo mpango ukianza kufanya kazi nishtue

Sorry but I can’t guarantee that

Kwani na wewe ni raia wa Uswiss?..

roman catholic,the mother of jesus bogus story

Hao clowns tu. Kazi yao ni kuchekesha watoto wanaokwenda kutembelea Vatican. Umeona wapi walinzi wakavaa kama Zwart Pit?

Udini mpaka UGENINI??

aisee, lakini labda wanaweza kupunguza Masharti mkuu, ila kazi zingine Yataka moyo, full utumwa

Zamani waswiswi walikuwa maskini sana. Nchi iko landlocked na milima mitupu. wengi walikuwa wanafanya kazi kama mamluki/mercenaries ili kujipatia kipato. walikuwa hodari sana wa vita. Hata papa aliwachukua kama walinzi wake. sasa kuna nyakati papa alishambuliwa na jeshi kubwa sana lakini walinzi wake/ waswiswi walisimama kidete hadi papa akafanikiwa kutoroka. Kwa tendo hilo la kishujaa hadi leo walinzi wa papa hutoka kwa waswiswi.

Unastaafu ukiwa 30

Nyabhingi; it is a historical fact Jesus of Nazareth did actually live on this earth and most of those written about him took place.
Tafuta vitabu vya historia (non-religious) utajionea ukweli huo. Ni vigumu sana mtu kutunga uongo na ukadumu especially when you consider the current level of technology.

Okay kumbe hawafanyi hiyo kazi hadi uzeeni.